ZOMBI NA WENZAKE WAHUKUMIWA 16/09/2016
UNAIKUMBUKA KESI YA ZOMBI...? HUKUMU IMETOLEWA IJUMAA 16/09/2016
Mahakama
ya Rufani imemhukumu kunyongwa hadi kufa aliyekuwa Mkuu wa upelelezi
wilaya ya Kinondoni (OC-CID), Mrakibu wa Polisi (SP) Christopher Bageni,
baada ya kumtia hatiani kwa kosa ka mauaji ya wafanyabiashara watatu wa
madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro.
Wakati
Bageni akihukumiwa kitanzi, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Dar
(RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na maafisa
wengine wawili wa Polisi, Ahmed Makelle na Rajabu Bakari wameachiwa
huru, baada ya mahakama kuwaona kuwa hawana hatia.
Bageni amehukumiwa adhabu hiyo leo baada ya mahakama ya Rufani kukubaliana na rufaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
DPP alikata rufaa akipinga hukumu ya Mahakama Kuu kuwaachia huru katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara hao.
chanzo: mpekuzihuru.com

0 comments: