HUU NDIO UKWELI KUHUSU MAMA ALIYEAMUA KUISHI UCHI JUU YA PAA LA NYUMBA HUKO MBEZI BEACH...!!

...................


WIKI iliyopita kuliibuka sakata zito lililochukua nafasi kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, lililomuhusisha mama mmoja aliyejulikana kwa jina la Hezelina Mrema mkazi wa Mbezi Beach, eneo la Tangi Bovu jijini Dar es Salaam, kuamua kuishi juu ya paa la iliyodaiwa kuwa ni nyumba yake.
Hatua hiyo ilisababisha baadhi ya wanaharakati kujitokeza na kuahidi kumsaidia mama huyo, aliyedai kuwa anataka kutolewa kwa nguvu ndani ya nyumba yake halali, ambayo ameijenga na mumewe Samwel Opulukwa.

UKWELI WA MAMBO

Ukweli juu ya suala hilo ni kwamba Hezelina hahusiki kwa namna yeyote na nyumba hiyo, ambayo ni ghorofa moja, kwani imebainika kuwa si mke halali wa Opulukwa na badala yake wana mahusiano ya kimapenzi.
Imebainika kuwa mke halali wa Opurukwa alisha achana nae na mke wake huyo tayari alishaweka pingamizi Mahakamani la kutaka hati ya nyumba hiyo isibadilishwe mmiliki.
Mbali ya Hazelina kutokuwa mke halali wa Opulukwa pia imebainika kwamba mwanaume huyo aliitumia nyumba hiyo kuweka dhamana ya mkopo kwenye benki ya TIB.

Imebainika kuwa hatua ya Opulukwa kuweka nyumba yake dhamana ilikuja baada ya rafiki yake ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Asasu Express Ltd kuhitaji fedha za kuendeshea bishara yake, lakini alikumbana na kikwazo cha kutakiwa kuwa na nyumba jijini Dar es Salaam, ambapo kwa kuwa hakuwa nayo aliona amtumie rafiki yake huyo kufanikisha mkopo wake kwa makubaliano kuwa ataulipa bila tatizo.

Hata hivyo mmiliki huyo wa kampuni ya Asasu alishindwa kulipa mkopo huo wa mamilioni ya fedha, ambapo benki husika ilianza harakati za kutaifisha mali zake ili kufidia deni hilo, hata hivyo hazikutosha na ndipo walipoamua kuiuza nyumba hiyo ya Mbezi Beach iliyopo kiwanja namba 235 Block D.
Imeelezwa kuwa benki ya TIB ilimpa Opulukwa taarifa zote za deni husika pamoja na kumpa Notisi ya kumtaka alipe deni husika ambalo ni 274,854, 256. 84 kutokana na rafiki yake kushindwa kulipa deni husika pamoja na mali zake kutaifishwa.

Ili kufuata taratibu za kisheria za kutaifisha nyumba ya Opulukwa, benki hiyo ilitoa tangazo la kutoa tenda ya kuuza nyumba hiyo, ambalo lilitolewa kwenye gazeti la serikali Januari 10,2011.
Hata hivyo Opulukwa hakutoa ushirikiano wowote, hali  iliyosababisha benki ya TIB kuipiga mnada nyumba hiyo na kufanikiwa kupata mteja, ambaye aliinunua kihalali ikiwa ni pamoja na kubadilisha hati miliki ya nyumba hiyo.
Jambo la kushangaza Opulukwa aliendelea kuishi ndani ya nyumba hiyo, TIB ilifanya harakati za kumtoa kwa kuyatumia makampuni kadhaa ya udalali ambayo yalishindwa kufanikisha kazi hiyo na ndipo Machi mwaka huu, jukumu hilo la kumtoa Opulukwa lilipelekwa kwa kampuni ya udalali ya Msama Auction Mart.

Baada ya Kampuni ya Msama Auction Mart kufanya taratibu zake za kikazi na kuridhishwa na uwepo wa deni husika, Juni 8, mwaka huu ilifika eneo la tukio na kuanza kumtoa Opulukwa.

Hata hivyo zoezi hilo lilikuwa gumu kutokana na baadhi ya maofisa wa Polisi wa Wilaya ya Kinondoni kuingilia kati, ambapo waliitisha kikao cha pamoja kati ya maofisa wa kampuni ya Msama Auction Mart na Opulukwa, ambapo maamuzi yalikuwa ni kusimamisha zoezi hilo hadi pale mkopaji huyo atakapopata baraka za Mahakama juu ya uhalali wa kuendelea kuishi kwenye nyumba hiyo.
Baada ya maamuzi hayo ya jeshi la polisi, Opulukwa alifungua kesi ya madai ya kuvunjiwa nyumba yake na kuibiwa vifaa vyenye thamani ya shiringi 195 milioni, jambo ambalo halikuwa na ukweli wowote.

Juni 11, mwaka huu mara baada ya Opulukwa kukosa vielelezo vilivyompa uhalali wa kuendelea kuishi ndani ya nyumba hiyo kama alivyoagizwa na Mkuu wa Polisi wilaya Kinondoni, kampuni ya Msama Auction Mart iliendelea na zoezi la kumuondoa.

Wakati maofisa wa kampuni ya Msama Auction Mart wakiwa na uhakika wa kukamilisha zoezi lao pamoja na kuondoka eneo hilo,ghafla walipigiwa simu na walinzi walioachwa kwenye eneo hilo kuwa kuna mtu yupo ndani ya nyumba, ambaye inaelezwa aliruka ukuta ili kufanikisha lengo lake.

Hatua hiyo ya Hazelina iliwashangaza maofisa wa Msama Auction Mart, ambao walichukua jukumu la kupiga simu polisi ili kuhakikisha mama huyo anaondolewa kwa njia ya amani na utulivu.
Wakati huo tayari Hazelina alikuwa ameshapanda juu ya paa la nyumba hiyo, huku akitishia kujirusha ili kuutoa uhai wake endapo angetolewa kwa nguvu.

Aidha alikwenda mbali zaidi kwa kuvua nguo ili kuonesha utupu wake, lengo lake likiwa ni kutowapa nafasi walinzi wa kiume kutomsogelea.

Hatua ya mama huyu kuonesha utupu wake na kuendelea kukaa juu ya paa la nyumba hiyo ilizua maswali na kuwafanya baadhi ya waandishi wa Habari kufika eneo hilo ili kujua ukweli wa mambo.

Kutokana na kauli za uongo za mama huyo, alifanikisha   kuwaaminisha waandishi wa habari kuwa kuna hila zinafanyika ili kupora nyumba yake, ambayo alidai kuwa ni halali yao.
Hata hivyo maamuzi ya mama huyo kuendelea kukaa juu ya paa la nyumba hiyo, yalidumu kwa muda wa siku mbili, ambapo Juni 13, mchana kwa hiyari yake aliamua kushuka baada ya kumuona jamaa yake akiwa ameshikilia karatasi zilizodaiwa kuwa zimetoka Mahakama ya Kinondoni.
Uchunguzi wa wetu umebaini kuwa Opulukwa hakumueleza ukweli mama huyo, ambapo ukweli halisi wa zoezi zima la kuhamishwa kwenye nyumba hiyo analijua.

Aidha imebainika kuwa mwanamama huyo si mke wa Opulukwa, kwani mke wake halali anajulikana kwa jina la Rachel Paulo Ng’wahi, amabaye ndiye aliyefungua kesi ya kupinga hatua ya mume wake kutumia nyumba yao kumuwekea dhamana ya mkopo rafiki yake ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Asasu.

Ukweli ni kwamba benki ya TIB na kampuni ya Msama Auction Mart, walikuwa sahihi kumuondoa Opulukwa kwenye nyumba hiyo, hakuna sheria yeyote waliyoivunja  na hawakuwa na nia ovu ya kutaka kumpora mama huyo  na Opulukwa aliyedai kuwa ni mumewe nyumba kama alivyodai kwenye vyombo vya habari.
 
chanzo:gumzo la jiji

http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: