Jaa la taka lageuka kitega uchumi Kenya
Takataka nyingi ya Nairobi hutupwa katika jaa la taka la Dandora, mtaani Dandora viungani mwa mji mkuu wa Kenya ,Nairobi. Harufu pekee ya eneo hilo hukera mno, lakini watu wa mtaa huu wamezoea mazingira yao.
Licha ya athari za mazingira haya, watoto hucheza hapa, karibu na maji taka bila kufahamu harati inayowazingira.
Kwa watu wengi wanaoishi karibu na jaa la taka mtaani Dandora, eneo hilo lenye taka limekuwa njia ya wao kujikimu kimaisha kwa kuokota takata mfano chupa na mikebe kisha kuziuzia kampuni za kutengeza plastiki.
Moja ya miradi ambayo, hufaidika kutokana na jaa la taka la Dandora ni mradi wa kutengeza mkaa mweupe ujulikanao kama Mukuru. Je wao huweza vipi kufanya hivyo? Wanatumia vipi jaa la taka kujikimu?
PICHA KWA NIABA YA WAIRIMU GITAHI BBC
0 comments: