Japan yaahidi msaada wa dola bilioni 32 kwa Afrika

...................
Japan imeahidi nchi za Afrika msaada wa dola bilioni 32  kuimarisha sekta za umma na kibinafsi ili kukuza ukuaji wa uchumi katika bara hilo.Msaada huo ambao utatolewa kwa kipindi cha miaka mitano ijayo utajumuisha msaada wa maendeleo kwa serikali za Afrika wa dola bilioni 14 ujulikanao kama ODA.Hayo yametangazwa kwenye mkutano wa siku tatu mjini Yokahama karibu na mji mkuu Tokyo nchini Japan ulioanza leo.Japani inajaribu kushindana na nchi jirani ya China ambayo ina ushawishi mkubwa barani Afrika kwa kufanya uwekezaji mkubwa katika miradi ya miundo mbinu.Waziri Mkuu wa Japani Shinzo Abe ambaye alichukua madaraka mwaka jana katika hotuba yake ya ufunguzi alipokutana na maafisa  kutoka nchi za Afrika zikiwemo Zimbabwe,Ghana,Sudan na Kenya amesema kile Afrika inachohitaji kwa sasa ni uwekezaji katika sekta ya kibinafsi.Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Japani miongoni mwa hatua nyengine za kuzisaidia nchi za Afrika ni pamoja na kuawachukua watu 1,000 kutoka Afrika kujifunza na kufanya kazi katika kampuni za Japani.

chanzo:Dw swahili http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: