Korea Kaskazini yafunguma mlango kwa Marekani

................... Korea Kaskazini imependekeza  mazungumzo ya ngazi ya juu kabisa na Marekani kwa lengo la kujadili mpango wa silaha za nyuklia na kuondoa mvutano kuhusu rasi ya korea. Katika taarifa yake Kamisheni yenye nguvu juu ya masuala wa taifa katika ulinzi, iliyotolewa na shirika la habari la taifa hilo imesema imependekeza mazungumzo hayo, kwa lengo la kuwezesha upatikanaji wa amani na utulivu katika kanda hiyo. Ikiitaka Marekani ipange muda na mahala yatakapofanyika. Kamisheni hiyo imeongeza kuwa Korea Kaskazini iko tayari kwa uwepo wa mazungumzo madhubuti katika uwanja mpana, likiwemo lengo la Marekani la kutokomeza matumizi ya nishati ya nyuklia duniani.

Na dw swahili http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: