Mawaziri wa NATO wazungumzia kuhusu gesi ya sumu iliyotumika Syria
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria Lakhdar Brahimi amesema leo kuwa mkutano wa kimataifa mjini Geneva haujapangiwa tarehe maalum kujadili mzozo nchini Syria , lakini kutakuwa na mkutano wa matayarisho utakaofanyika Juni 25.Brahimi aliyasema hayo baada ya kukutana mjini Geneva na maafisa wa Marekani na Urusi kuzungumzia maandalizi.
Wakati huo huo taarifa mpya kwamba Ufaransa imethibitisha matumizi ya gesi ya Sarin nchini Syria zimezusha majadiliano pembezoni mwa mkutano wa mawaziri wa ulinzi wa NATO mjini Brussels , lakini umoja huo bado unasita kuamua mipango kamili kwa ajili ya operesheni nchini humo. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Laurent Fabius amesema serikali ya Syria inabeba lawama za mashambulio hayo.
Wakati huo huo waasi nchini Syria wamekiri kuwa wameupoteza mji muhimu wa Qusayr baada ya kuudhibiti kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Na dw swahili
0 comments: