Shirika la Msalaba Mwekundu lahimiza raia waachiwe kuyahama maeneo ya mapigano
Mapigano yamepamba moto katika mji wa Qusair. Mamia ya majeruhi hawana njia ya kupatiwa matibabu.Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu limezitolea wito pande zinazohasimiana ziwaruhusu wauguzi wawafikie majeruhi bila ya masharti.Duru kutoka Geneva zinasema watumishi wa Shirika la Hilali Nyekundu wanasemekana wako tayari kwenda Qusair kusaidia.Kabla ya hapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alizitolea wito pande zinazohasimiana ziwaruhusu raia wayahame maeneo ya mapigano."Pande zinazohusika zinabidi zitambue ulimwengu unawaangalia na watalazimika kujibu uhalifu wanaowafanyia raia-amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.Wakati huo huo mkutano wa kusaka ufumbuzi wa mzozo wa Syria huenda ukaitishwa mwezi ujao wa July.
Na Dw swahili
0 comments: