TUSI LA PAUL KAGAME KWA RAIS KIKWETE
MATUSI ya Rais wa Rwanda Paul Kagame kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano
wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jakaya
Mrisho Kikwete yamewagawa Watanzania na kuwafanya wawe na mitazamo tofauti.
Wapo wanaomuunga mkono Rais Kagame na wapo pia wanaompinga kwa kauli yake...
Rais Kagame alimtukana Rais Kiwete kwa kuita ushauri wake kwamba ni
ushauri wa kijinga kwa wanyarandwa,awali Rais Kikwete alizishauri nchi
za Rwanda na Congo DRC kukutana na kumaliza tofauti zao kwa njia ya
amani.
Rais Kikwete alitoa ushauri huo wakati wa mkutano wa kujadili amani
na mpango wa ulinzi nchini Congo DRC uliofanyika katika Makao Makuu ya
AU mjini Addis Ababa Ethiopia.
Katika ushauri huo Rais Kikwete alisema kwamba ni vyema Rais Kagame
akakaa katika meza ya mazungumzo ya amani na Rais wa Congo DRC Joseph
Kabila ili kumaliza tofauti zao badala ya kutumia nguvu ya kijeshi.
“Nimekaa kimya kwa kipindi kirefu
na kwa jinsi nilivyoweza kwa sababu nilifikiri kwamba mazungumzo ya
kipuuzi yaliyozungumzwa na watu wajinga yamemalizika "alisema Rais
Kagame.
Katika hatua nyingine Rais Kagame
alisema kwamba ushauri huo wa Rais Kikwete ni sawa na kuwachezea
wanyarandwa mbele ya mataifa.
Rais
Kagame aliyasema hayo katika sherehe ya kuhitimu mafunzo ya maofisa wa
jeshi wapatao 45 katika kituo cha mafunzo ya kijeshi siku ya Juma Tatu
nchini Rwanda.
chanzo:unapitwa
0 comments: