Du huyu alipinda hadi kuitwa........
Mbakaji sugu Afrika Kusini afariki
Mwanamume anayetuhumiwa kuwa
mbakaji sugu nchini Afrika Kusini ,Sifiso Makhubo, amepatikana akiwa
amefariki katika chumba chake gerezani.
Sifiso Makhubo, aliyekuwa anakabiliwa na mashtaka 122 ikiwemo mauaji na ubakaji alipatikana akiwa amejinyonga kwa blanketi.Afrika Kusini ina moja ya visa vingi zaidi vya ubakaji duniani, huku polisi wakionyesha kuwa ni visa 64,000 pekee ambavyo viliripotiwa mwaka jana.
Maafisa wanasema kuwa alikuwa peke yake katika seli yake , lakini wanachunguza kilichosababisha kifo chake.
Bwana Makhubo anatuhumiwa kwa kuwabaka watoto 35 na wanawake wawili, kati ya Januari mwaka 2006 na Februari 2011.
Hadi sasa uchunguzi uliofanywa wa DNA katika waathiriwa waliodai kubakwa naye, ulithibitisha kuwa yeye ndiye alikuwa mbakaji
chanzo:bbcswahili
0 comments: