Hatimaye Abu Qatada afikishwa Jordan.
Abu Qatada akipanda ndege wakati anaondoka.
Mahakama nchini Jordan
imeshitaki Muhubiri wa Kiislamu Abu Qatada kwa makosa yanayohusiana na
Ugaidi baada ya kurejeshwa nchini Humo akitokea Uingereza mapema hii
leo.
Mashitaka ya kesi hiyo yamefuata yale ya mwaka 1999 dhidi yake.Kufika kwa Abu Qatada nchini Jordan kumemaliza mabishano ya kisheria ya miaka nane ya serikali ya Uingereza kutaka kumrejesha nchini Jordan,
Mabishano ambayo yameigharimu serikali ya Uingereza kiasi cha pound milioni mbili na nusu fedha za walipa kodi.
Mwandishi wa BBC mjini Amman amesema licha ya ahadi ya serikali ya Jordan ya kuendesha kesi hiyo kwa uwazi na usawa, lakini wanahabari wamezuiliwa kuingia mahakamani kusikiliza kesi hiyo
chanzo:bbcswahili

0 comments: