MFAHAMU ATAKAYEKUWA WAZIRI MKUU WA MUDA WA MISRI
ElBaradei kuwa waziri mkuu wa Muda, Misri
Kiongozi mkuu mwenye siasa za wastani Mohammed El Baradei anatarajiwa kutangazwa kama waziri mkuu wa mpito nchini Misri. El Baradei ni mkuu wa zamani wa shirika la masuala ya Nyuklia la Umoja wa Mataifa na pia mwanaharakati wa Upinzani.Kwa mujibu wa shirika la habari la taifa Al Mena, Baradei hapo jana alikutana na rais wa muda Adly Mansoor. Hata hivyo hatua ya Mohammed Baradei kupewa cheo cha waziri mkuu imezua maandamano makubwa kutoka kwa wafuasi wa rais aliyepinduliwa madarakani Mohammed Mursi.
Huku hayo yakiarifiwa hapo jana rais wa Marekani Barack Obama amesema nchi yake haiungi mkono chama chochote cha kisiasa nchini Misri wala kundi lolote. Obama amelaani ghasia zinazoendelea katika maeneo tofauti nchini humo.
Siku ya Ijumaa wafuasi wa Mursi pamoja na wapinzani wake walikabiliana vikali na kusababisha vifo vya watu 35 huku zaidi ya 1000 wakiwa wamejeruhiwa.

0 comments: