Madaktari wa Mandela wabadili msimamo wa kuzima mashine
Kwa ufupi
Madaktari hao, wameishauri familia hiyo kuachana na
ushauri wa awali wa kuindoa mashine hiyo, hadi tu pale moja ya kiungo
chake muhimu cha mwili kitakaposhindwa kufanya kazi.
Johannesburg. Madaktari wanaomtibu Rais wa
zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, wamebadili msimamo wao wa awali
wa kuiondoa mashine inayomsaidia kupumua kiongozi huyo, kwa maelezo
kuwa hali yake si mahututi.
Madaktari hao, wameishauri familia hiyo kuachana
na ushauri wa awali wa kuindoa mashine hiyo, hadi tu pale moja ya kiungo
chake muhimu cha mwili kitakaposhindwa kufanya kazi.
Mmoja wa marafiki wa karibu na mpigania uhuru
ambaye aliwahi kufungwa pamoja na Mandela, Denis Goldberg, amesema
madaktari hao waligusia kuhusu suala la kuondoa mashine lakini baadaye
walikataa kwa kuwa Rais huyo hayuko katika hali mbaya kiasi cha kukata
tamaa.
Goldberg alieleza kuwa Mandela ana uwezo wa kupata nafuu, kwani anaweza kusogeza baadhi ya viungo na kutambua sauti.
Juzi vyombo vya habari vya hapa nchini vilitoa
hati ya kiapo ya Mahakama, ikionyesha kuwa madaktari hao waliishauri
familia ya Mandela kuondoa mashine ya kumsaidia kupumua kwani,
‘asingeweza kuendelea kuishi’.
Sintofahamu
Taarifa hizi zimekuja wakati ambapo wanafamilia ya
Mandela ambao walikwenda mahakamani kwa ajili ya kesi ya kufukua miili
ya watoto watatu wa Mandela kuandika katika ripoti ya Mahakama kuwa Rais
huyo alikuwa mahututi.
“Ni kweli kuwa hali ya Mandela ni mbaya, lakini si
kama ambavyo baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikiandika” alisema
Goldberg.
Ushuhuda wa mwisho uliotolewa na wanafamilia hiyo
mahakamani, umedaiwa kuwa ulikuwa ni mbinu tu ya kuharakisha hukumu
dhidi ya mjukuu wa Mandela, Mandla.
Kauli ya kuwa hali ya Mandela ilitiwa chumvi ili
kuharakisha hukumu ya Mahakama, imetolewa wakati Ofisi ya Rais ya Afrika
Kusini ilipoitaka familia hiyo kutatua mgogoro wa maziko.
“Inasikitisha kuwa kuna mgogoro katika familia
hiyo na tungependa utatuliwe mapema iwezekanavyo” alisema msemaji wa
Rais Jacob Zuma, Mac Maharaj jana.
Hata hivyo, Maharaj alikataa kuzungumzia kuhusu
hati ya Mahakama ambayo ilieleza kuwa Rais huyo wa zamani mwenye miaka
94, yupo mahututi na kuwa madaktari wameshawashauri wanandugu kuondoa
mashine ya kupumulia.
chanzo:unapitwa.com
chanzo:unapitwa.com

0 comments: