VIJIMAMBO VYA MJUKUU WAKATI MANDELA AKIWA HOSPITAL
Mandla ashindwa katika kesi ya makaburi
Mjukuu wa Nelson Mandela, Mandla
Mandela ameshindwa katika kesi iliyowasilishwa mahakamani dhidi yake
kwa tuhuma za kufukua makaburi ya jamaa za familia yake katika mzozo wa
makaburi unaokumba familia ya Mandela.
Mgogoro huo unahusu maiti za wanawe Mandela
watatu ambao Mandla alihamisha na kuwazika karibu na nyumbani kwake
zaidi ya miaka miwili iliyopita.Mandela anaendelea kuugua hospitalini na haijulikani ikiwa mawakili wa Mandla wataka rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama.
Jamaa za familia ya Mandela waliwasilisha kesi ya uhalifu dhidi ya Mandla kwa kosa la uhalifu.
Msemaji wa polisi, Mzukisi Fatyela aliambia BBC kuwa maafisa wa usalama watachunguza tuhuma dhidi ya Mandla za kufukua makaburi kinyume na sheria
Inahusisha maiti za watoto watatu wa Mandela ambao inaaminika walifukuliwa na Mandla kutoka makaburi ya familia miaka miwili iliyopita.
Familia ya Mandela, inataka kurejesha miili hiyo katika kijiji cha Qunu, ambako Mandela, ambaye anaumwa sana hospitalini anataka kuzikwa akifa.
Kesi hiyo iliyosikilizwa katika mahakama kuu ya Mthatha, katika mkoa wa Mashariki iliakhirishwa hapo jana lakini hukumu ikitaolewa Jumatano.
Wiki jana, mahakama ilitoa amri ya muda kwa maiti za watatu hao kuhamishwa kutoka nyumbani kwa Mandla katika kijiji cha Mvezo hadi Qunu, umbali wa kilomiya 22.
Lakini Mandla Mandela, ambaye alitawazwa kama kiongozi wa kijamii na babu yake, sasa anapinga vikali amri hiyo.
chanzo:bbcswahil
0 comments: