AU yapitisha azimio kuhusu ICC
Viongozi wa Afrika waliokuwa
wakikutana mjini Addis Ababa, Ethiopia, wamekubaliana kuwa Rais Uhuru
Kenyatta wa Kenya asihudhurie kesi yake katika Mahakama ya Jinai ya
Kimataifa, ICC, ila ikiwa itaakhirishwa.
Katika azimio lao viongozi wa Afrika walisema
kuwa kiongozi yeyote wa taifa asitakiwe kuhudhuria mahakama yoyote ya
kimataifa wakati yuko madarakani.Bwana Kenyatta siku zote amesema kwamba atashirikiana kikamilifu na ICC.
AU inaishutumu ICC kuwa na kigeugeu - kwamba inawashtaki Waafrika na siyo watu wa mataifa ya magharibi.
Hapo awali Waziri Mkuu wa Ethiopia, Hailemariam Dessalegn, alisema kesi za ICC dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta na Omar al-Bashir wa Sudan zinaweza kuzuwia juhudi za kuleta amani na mapatano katika nchi zao.
Mkutano umemalizika.
CREDIT:bbcswahili
0 comments: