MWAMAMKE ALIJIFUNGUA MAPACHA WANNE MBEYA, AOMBA MSAADA KWA WASAMARIA WEMA.
MWAMAMKE ALIYEJIFUNGUA MAPACHA WANNE AOMBA MSAADA KWA WASAMARIA WEMA HUKO MBEYA.
Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya
Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne mapacha kwa
mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea
vizuri.
Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu
katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne
alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi
Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito
wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi.
Muuguzi na msimamizi wa Watoto katika chumba cha Joto Sista
Frolence Maisa amesema hali za watoto ni nzuri ambapo mama mzazi
anahitaji kupatiwa vyakula vinavyoweza kumuongezea maziwa mengi kutokana
na idadi ya watoto aliyonayo.
kikosi cha blog ya Mbeya yetu Kikiongozwa na Joseph
Mwaisango ambacho kilifika kumjulia hali kiliguswa na hali hiyo na
kujitolea kamsaada kidogo wa nguo za watoto sabuni chupa na dishi
hivyo kuwaomba wadau wengine kumsaidia mama huyo ili aweze kuwalea
vizuri watoto wake.Katibu msaidizi wa hospitali ya Rufaa Mbeya Mwansasu
akipokea msaada huo kwa niaba ya mzaziKATIKA hali isiyokuwa ya Kawaida
Mwanamke mmoja, Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya
Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne mapacha kwa
mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea
vizuri.
'Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu
katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne
alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi
Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito
wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi.
Kwa mujibu wa Muguuzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbozi
aliyemfanyia huduma mwanamke huyo, Grace Konga alisema mzazi huyo ni
miongoni mwa wazazi 9 waliojifungua katika Mkesha wa Mwaka mpya huku
yeye akivunja rekodi kwa kujifungua watoto wanne kwa njia ya
kawaida. Muuguzi huyo alisema watoto hao walizaliwa wakiwa na uzito
uliotofautiana kwa mtoto wa kwanza hadi wa mwisho kuanzia kilogramu
1.6,1.5,1.5 na 2.0 ambapo baada ya kuona hali hiyo ilibidi kumpa rufaa
kwa ajili ya msaada zaidi katika Hospitali ya wazazi ya Meta ambapo
wapo katika Chumba cha Joto hadi sasa.
Aidha kwa mujibu wa Muuguzi na msimamizi wa Watoto katika
chumba cha Joto Sista Frolence Maisa amesema hali za watoto ni nzuri
ambapo mama mzazi anahitaji kupatiwa vyakula vinavyoweza kumuongezea
maziwa mengi kutokana na idadi ya watoto aliyonayo. Alisema kwa hivi
sasa watoto wananyonya vizuri amb po maziwa yakipungua kwa mama
itahitajika msaada wa maziwa ya Kopo aina ya Laktojeni ili watoto
waendelee kupatiwa maziwa kama kawaida na afya zao kuimarika.
Kwa upande wake Mzazi wa watoto hao Aida Nakawala alisema
hali yake kiuchumi siyo nzuri kuweza kumudu kuwalea watoto hao na
kuongeza kuwa mume wake ni mkulima aliyemtaja kwa jina la Web Simkanda
hivyo anaomba msaada wa hali na mali kutoka kwa wasamaria wema.Alisema
huo ni uzao wake wanne ambapo mtoto wake wa kwanza anaumri wa miaka
saba, anayefuata ana miaka miwili na miezi tisa huku mwingine akiwa
amefariki dunia mara baada ya kujifungua kabla ya uzao huu unaofanya
kuwa na watoto Sita.Alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa hali kama hiyo ya
kujifungua watoto zaidi ya mmoja katika familia yao alisema Mama yake
mzazi amewahi kujifungua mapacha wawili tu na hakuna mtu mwingine
aliyewahi kuzidisha idadi hiyo ya watoto kama yeye .
Hata hivyo kutokana na kuguswa kwa mahitaji ya binti huyo
na wanawe kikosi cha blog ya Mbeya yetu ambacho kilifika kumju ulia hali
kiliguswa na hali hiyo na kujitolea kamsaada kadogo hivyo kuwaomba
wadau wengine kumsaidia mama huyo ili aweze kuwalea vizuri watoto wake.
credit:mute

0 comments: