SHETANI WA MTU NI MTU:MFANYABIASHARA WA KIKE APIGWA RISASI USONI NA KUPORWA MABEGI MAWILI YA FEDHA KARIAKOO.
MFANYABIASHARA WA KIKE APIGWA RISASI USONI NA KUPORWA MABEGI MAWILI YA FEDHA KARIAKOO.
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI
ZENYE KUSIKITISHA SANA.
Mwili wa mfanyabiashara huyo ukiwa kwenye gari mara baada ya kupigwa risasi na majambazi (majira ya saa 12 Kasoro jioni) Damu ya Mfanyabiashara huyo ikiwa imetapakaa katika gari lake baada ya kupigwa risasi na majambazi waliompora kiasi kikubwa cha fedha na kutoweka.
ZENYE KUSIKITISHA SANA.
Mwili wa mfanyabiashara huyo ukiwa kwenye gari mara baada ya kupigwa risasi na majambazi (majira ya saa 12 Kasoro jioni) Damu ya Mfanyabiashara huyo ikiwa imetapakaa katika gari lake baada ya kupigwa risasi na majambazi waliompora kiasi kikubwa cha fedha na kutoweka.
Raia wakishangaa mwili wa mfayabiashara huo ukiondolowa na
polisiAskari wakiliondoa gari la mfanya biashara huyo katika eneo la
tukioEFD machine ikiwa katika gari la mfanyabiashara aliyepigwa risasi
leo jijini Dar es SalaamSehemu ya fremu inayosemekana kuwa ni Duka la
mfanyabiashara aliyepigwa Risasi Leo majira ya saa 12
jioniMfanyabiashara mmoja (Jina Halikufahamika) Mwenye asili ya Asia
ameshambuliwa na majabazi (majira ya saa 12 Kasoro jioni )kwa kupigwa
risasi katika paji la uso wake na kisha majambazi hao kutoweka na mabegi
mawili yaliyoojaa fedha.Hata hivyo haikujulikana kwa haraka ni kiasi
gani cha fedha ambacho kilikuwemo katika mabegi hayo.
Wakiongea na mwandishi wetu baadhi ya mashuhuda wa tukio
walidai kuwa majambazi hao walikuwa watatu na mmoja alikuwa na bunduki
aina ya SMG. Wakielezea tukio hilo baadhi ya wafanyabiashara wengine
katika maeneo hayo ya mtaa wa Lindi na Kongo (Kariakoo) walidai kwamba
Mfanyabiashara huyo alitoka na kufunga duka lake huku akiwa na mabegi
mawili na Mashine ya kutolea Risiti ya EFD na kuelekea katika gari lake
dogo aina ya Suzuki Carry na Ghafla walitokea watu wawili waliokuwa
katika pikipiki na mmoja wa tatu alikuwa amesimama pembeni kidogo na
gari hiyo na kisha kuelekea moja kwa moja katika gari hiyo na kumpiga
risasi mfanya biashara huyo aliyekuwa akijiandaa kuondosha gari lake.
'Niliona watu kama wanagombania begi hivi ghafla nikasikia
mlio wa risasi na kisha nikaona pikipiki mbili aina ya boxer zikija kwa
kasi kutokea upande wa mtaa wa gerezani na kisha mlio wa pili wa
risasi ulikika tena, nahisi ndio uliokuwa umemlenga yule "muhindi" na
baada ya hapo kitendo kama cha dakika mbili hivi wale jamaa wakapokezana
lile begi na kisha kupiga risasi nyingine juu basi hapo wote tukaanza
kufunga maduka yetu na wale majambazi wakatoweka kirahisiii"Hata hivyo
baadhi ya watu wamelaumu utaratibu wa wafanya biashara wengi wa kariakoo
kuhifadhi fedha nyingi katika maduka na badala yake wamewataka wafanya
biashara hao kutafuta mbinu mbadala itakayowaezesha kuweka fedha na mali
zao salama kabisa ikiwa ni pamoja na kutumia huduma za kuhamisha fedha
kwa kutumia mitandao, cheque, na hata credit card kuliko Cash kwani
imekuwa kawaida kwa mtukio haya kujirudia eneo hili la Kariakoo.

0 comments: