DAAAA...HII MPYA:ASKOFU AZIKWA KAMA YESU, TAZAMA PICHA
Askofu wa dayosisi ya Malindi Emmanuel Barbara akiongoza mazishi ya
Askofu Boniface Lele katika kanisa la Holy Ghost Cathedral Malindi
Aprili 22, 2014. Picha/LABAN WALLOGA.
Na MWAKERA MWAJEFA Na DANIEL NYASSY.
ASKOFU Mkuu Mstaafu Boniface Lele jana
alasiri alizikwa kwa kuzingatia tamaduni zote za Kanisa Katoliki katika
uwanja wa Holy Ghost Cathedral, Mombasa.
Lakini
mazishi ya askofu huyo yalikuwa ya aina yake huku kaburi lake likifanana
na lile alimozikwa Yesu na watu wengine wa enzi hizo.
Pango dogo lilichimbwa
kwenye mwamba kutoshea jeneza la marehemu na hakuna hata punje ya
mchanga iliyotupwa kaburini humo kama ilivyo kawaida katika mazishi ya
kisasa.
Baada ya maombi maalumu kando ya pango hilo dogo, jeneza lilisukumwa ndani kisha pango hilo likafunikwa kwa simiti na vyuma.
Kulikuwa na ulinzi mkali kabla ya jeneza la marehemu kuletwa kutoka katika shule ya Loreto ilikofanywa ibada ya wafu.
Umati mkubwa wa watu ulisongamana nje ya kanisa hilo wakitaka kuingia ndani lakini walinzi waliwazuia hadi mwili ulipoletwa.
Polisi wa
kawaida, wenzao wa utawala na wengi waliovalia kiraia walionekana juu ya
mapaa ya majumba yaliyo karibu na kanisa hilo kama vile Ambalal, TSS
Tower na Electricity House huku wengine wengine wakiwa chini.
Mwili
ulipofika ulipelekwa moja kwa moja hadi eneo la timbo la mawe
yaliyotumiwa kujenga jumba la makasisi na kuwekwa kwenye kivuli kusubiri
wakuu wa kanisa kutoka huko Loreto.
Wanahabari walizuiwa kukaribia eneo la timbo kwa hofu kwamba mawe yangeporomoka kutokana na uzito mkubwa juu.
Lakini baadaye ilithibitishwa kuwa mwamba huo ni imara na wanahabari wakaruhusiwa kukaribia.
Askofu
mwandamizi wa Jimbo la Malindi Kasisi Emmanuel Barbara aliwasili na
maaskofu wengine na wakateremka kwenye timbo hilo kuanza sherehe hiyo.
Jeneza
lilikuwa limeteremshwa na wanachama wa chama cha wanaume cha kanisa hilo
na kuwekwa kando na pango alimopumzishwa Askofu Lele.
Askofu Barbara akisaidiwa na mapadri aliongoza maombi ya mwisho kuombea roho ya marehemu ilale mahali pema peponi.
Alinyunyizia maji matakatifu mwili ukiwa ndani ya jeneza na kuufukiza ubani kwa mujibuni wa desturi za Kanisa Katoliki.
“Tukimuaga
ndugu yetu Askofu Emeritus Boniface Lele, tunajua ameenda kumuona Baba
Mungu uso kwa uso nasi tunatumai kujiunga naye katika ufalme wa milele
kwa baba,” akamaliza Askofu Barbara.
Vyuma
Baada ya sherehe hiyo fupi, maaskofu, mapadri na watawa waliwapisha Wakristo wengine ili watoe heshima zao za mwisho.
Hatimaye jeneza liliwekwa pangoni na waumini wakakafuatana kwa foleni na kupita karibu nalo huku wakitoa heshima za mwisho.
Walipomaliza, mafundi waliitwa na wakaanza kufunga kwa vyuma kwenye kiingilio cha pango.
Waziri wa
Ardhi, Bi Charity Ngilu ambaye alisoma hotuba ya Rais Uhuru Kenyatta,
alishangaza wengi alipomkumbatia hasimu wake wa kisiasa Kalonzo Musyoka
huku umati ukishangilia.
credit:eddy

0 comments: