ILIYOSHIKA HEADLINE:DUDU BAYA AMKATA SIKIO MAMA YAKE, KWA SASA ANASAKWA NA POLISI
Msanii mkongwe wa
Muziki wa Bongo Flava Godfrey Tumaini Maarufu kwa jina la DUDU BAYA /
MAMBA ameingia kwenye List ya wahalifu wanaotafutwa na jeshi la polisi
jijini Mwanza,
Taarifa
hiyo imekuja baada ya kusemekana kuwa eti juzi alidhihirisha kuwa yeye
ni DuduBaya baada ya kumvamia mama yake mkubwa na kumkata sikio lake,
Akisimulia mkasa huo Mdogo wake Dudu tumbo moja anayeitwa MUETA amesema
Juzi majira ya saa nne asubuhi jijini Mwanza DuduBaya alienda kwa mama
yake mkubwa ambaye alikua anaumwa sana kutokana na uzee,
Dudu
alipofika pale alimuita mama yake mkubwa na hakuitikiwa ndipo
alipomkokota mama yake mkubwa kutoka kibarazani nje na kumuingiza ndani
sebuleni akamlaza kwenye kochi na kuanza kumkata sikio lakini
hakufanikiwa kuling'oa lote kwasababu mama mkubwa alipiga kelele kuita
majirani ndipo Dudubaya akatoka nje na kutokomea kusikojulikana, lakini
wakati Dudu anafanya yote hayo mule ndani alikuwepo mtoto mmoja mdogo
ambaye hakuweza kumzuia mjomba wake asifanye ukatili huo,
Majirani
wakafika na kutoa msaada wa kwanza kwa bi Mkubwa na kumwahisha
Hospitali ya Sekeu Toure akashonwa sikio, kwani sikio hilo halikukatika
kabisa kwa sababu kisu alichokua anatumia Dudubaya kilikua butu,
Kwa Mujibu wa Mdogo wa Dudubaya "Mueta" anasema eti Dudu anamtuhumu mama yake mkubwa kuwa ni mchawi na anamroga.
Tukio hili limeripotiwa polisi na DuduBaya anatafutwa na polisi kwa Udi na Uvumba.
Chanzo: U Heard ya Clouds fm

0 comments: