HII KALI WEWE UNGEWEZA........!
Mtuhumiwa wa ubakaji ataka kubaka tena ndani ya jengo la mahakama
Imetokea
Kenya ambapo Simon Ngozi (21) alikuwa amepelekwa Mahakamani Makadara
Nairobi lakini ghafla akamshangaza kila mtu baada ya kutaka kumaka
Mwanamke aliekua karibu yake baada ya kuanza kumshikashika.
Mshukiwa huyu alikuwa
kortini kujibu tuhuma za kumbaka mtoto wa miaka tisa April 2014 ambapo
wakati anataka kumbaka Mwanamke huyu Mahakamani tena kwenye eneo la
wazi, alimpiga mtama kwanza Mwanamke huyo lakini kwenye purukushani zake
hakufanikiwa manake Polisi walimuwahi.
Shughuli za Mahakama
zilisimama kwa muda baada ya tukio hilo kutokea ambapo baada ya hapo
Mwanamke alietaka kubakwa alisema ‘nilikua nimeketi karibu naye na mara
ya kwanza alilishika begi langu nikalisogeza mbali nikidhani ni mwizi
lakini bila aibu akanishikashika tumboni kabla ya kunisukuma nikaanguka
sakafuni
Baada ya hapo dada wa
mtuhumiwa alimuomba mwanamke huyo kumsamehe ndugu yake akisema yuko
katika hali hiyo baada ya mchumba wake kumtoroka kwa sababu ya kesi ya
ubakaji.
CHANZO:MATUKIO NA VIJANA

0 comments: