Unabishaaaa!Lazio wasema Minala ana miaka 17 sio 42
Lazio; Minala ana miaka 17 sio 42
Uchunguzi wa shirikisho la soka
la Italia umebaini kuwa mchezaji tineja wa Cameroun Joseph Minala ana
umri wa miaka 17 wala sio 42 kama ilivyodhaniwa na kuripotiwa katika
vyombo vya habari.
Mnamo mwezi Februari mtandao mmoja wa michezo
barani Afrika ulichapisha habari ambayo ilizua dukuduku iwapo kiungo
huyo alikuwa amedanganya umri wake .Mtandao huo ulichapisha habari za kuashiria kuwa hakuwa tineja bali mtu mwenye umri wa miaka 42.
Lazio; Minala ana miaka 17 sio 42
Minala alijiunga na klabu hiyo yenye makao yake mjini Rome na hata alishiriki mchuano wa vijana wasiozidi umri wa miaka 23 wa Viareggio mnamo mwezi wa Februari
chanzo:bbcswahili

0 comments: