Atafuna Moyo wa adui wake A.Kusini
Polisi nchini Afrika Kusini
wanachunguza tukio ambapo mwanamume mmoja anaripotiwa kumuaa mwanamue
mwingine aliyekuwa na uhusiano na kimapenzi na mwanamuke anayeaminika
kuwa mpenzi wake w zamani.
Alimuua ka kumkatakata vipande na kisha kuula Moyo wake.Walioshuhudia wanasema kuwa wakati walipofika katika mtaa wa kifaharai ambako mshukiwa alikuwa anaishi walimsikia akisema kuwa "ni yeye mfalme" akisema kuwa bado anampenda mpenzi wake wa zamani.
Kwa sasa anazuiliwa na polisi
Polisi mmoja aliiambia BBC kuwa wakati walipowasili eneo la tukio walimpata mshukiwa akila moyo wa binadamu akitumia uma na kisu.
Walifahamishwa kuwa mwathiriwa alidungwa kisu upande wake wa kushoto kifuani na kwenye shingo lake na katika sehemu ya uso alikuwa na alama ya kuumwa.
Marehemu anayeaminika kuwa Bwana Mbuyiselo Manona,alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke aliyekuwa mpenzi wa mshukiwa kwa miaka minne.
Hapakuwa na dalili zozote za mwanamke huyo nyumbani kwake Jumatano lakini gari lake lilikuwa limeegeshwa nyumbani kwake.
Inaripotiwa si mara ya kwanza mwanamke huyo ambaye anasemekana kuwa na umri wa miaka 50 kuhusishwa na visa vinavyohusiana na mapenzi. Mumewe aliuawa na mtu anayekisiwa kuwa mpenziwe mwaka 1996
chanzo:bbcswahili
0 comments: