Facebook yakosolewa kuhusu fedha za Assad

...................



Kampeni ya Assad
Shirika moja la misaada limeitaka Facebook kurudisha fedha ilizopata kwa kufanya matangazo ya kampeni yake rais Bashar al-Assad wa Syria.
Matangazo hayo- ambayo sasa yametolewa na Facebook- yalianzishwa mwezi Mei , na yamehusishwa na ukurasa unaoitwa Sawa al-Assad. Sawa ina maana ya “pamoja”, neno ambalo alitumia rais huyo kama kauli mbiu wakati wa kampeni.

Utata umetokana na matangazo mengi yanayoendelea kuukuza katika mtandao wa Facebook. Kwa kuwa matangazo haya yalikuwa yamelipiwa, kampuni hiyo basi ilipokea fedha kwa matangazo hayo yaliyoimarisha kampeni ya siasa zake Assad- jambo ambalo limelikera shirika la kutoa msaada liitwalo ‘the Syria Compaign’.
Shirika hilo limetengeneza wavuti unaoitwa 'AdsForDictators.org unaokejeli Facebook' na unatoa malalamishi kwenye mtandao.
“Wanafanya pesa mbovu kuwa nzuri,” John Jackson ambaye ni mkurugenzi wa shirika hilo aliiambia BBC. “Wanapaswa kutoa pesa hizo kwa shirika la misaada lenye sifa ambalo linawashughulikia wakimbizi wa Syria.”
Haijulikani ni pesa ngapi, ingawa katika muda mfupi ambao tangazo hilo lilifanywa, kuna uwezekano kuwa ni kiwango kikubwa cha pesa.
Facebook bado haijasema chochote kuhusiana na jambo hilo, ila tu kusema kwamba tangazo hilo halikufanywa kutoka Syria- jambo ambalo litavunja masharti yaliyowekewa taifa hilo- na kwamba “kama kawaida sisi huondoa matangazo yasiyofuata kanuni zetu.”
Hata hivyo, haijulikani hasa ni kanuni zipi walizokiuka. Hakuna kabila lililotumiwa ambalo lina uchochezi, na pia matangazo ya kisiasa katika mtandao wa Facebook hukubaliwa.
Itakumbukwa kuwa kampuni hiyo ilikuwa imeorodhesha mbinu za kuwasaidia waliokuwa wakigombea nyadhifa mbalimbali mwaka wa 2012 nchini Marekani kupitia kwenye Facebook

chanzo:bbcswahili
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: