Ribery nje ya Kombe la Dunia
Mkufunzi wa Ufaransa amedhibitisha kuwa mshambulizi Frank Ribery hatashiriki kombe la dunia kutokana na jeraha.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 na
anayechezea klabu ya Bayern Munich alijeruhiwa mgongoni wakati wa
mazoezi siku ya Ijumaa.‘’Hataweza kufanya mazoezi wala kucheza kwa majuma kadhaa.”
Kiungo cha kati wa Southampton Morgan Schneiderlin na mshambulizi wa Montpellier Remy Cabella wamejumuishwa kikosini ili kucheza kwa niaba ya wawili hao.
Ribery alipelekwa kupigwa picha ya MRI, ambayo ilidhibitisha kiwango cha jeraha hilo.
Riberi alichaguliwa kuwa mchezaji wa tatu bora zaidi duniani mwaka wa 2013 nyuma ya mshindi wa Ballon d’Or Christiano Ronaldo wa Real Madrid na mshambulizi wa Barcelona Lionel Messi.
chanzo:bbcswahili
0 comments: