KAULI YA SERIKALI BUNGENI KUHUSU PICHA CHAFU MTANDAONI
Sakata la kusambaa picha zisizokuwa na maadili mitandaoni zikiwemo za watu maarufu hapa nchini leo limezungumziwa tena katika bunge la Tanzania kule Dodoma ambapo katika kipindi cha maswali na
majibu
Mhe. Habib Mnyaa ameonekana akihoji serikali inachukua hatua gani juu
ya watu wanaotuma picha zao zisizo na maadili mitandani zikiwemo za
kina Wema na Diamond wanazopiga wakiwa chumbani na kuweka kwenye
mitandao.
Katika majibu yake waziri wa
mawasiliano, sayansi na teknolojia Prof. Makame Mbarawa anasema “Mhe.
Spika kuhusu picha zisizokuwa na maadili zinazowekwa katika mitandao na
watu maarufu na hata wasiokuwa maarufu serikali imeanza kuandaa kanuni
zitakazokuwa zikifuatilia Online Content ambapo itaanza kuchukua hatua
baada ya kufuatilia juu ya picha hizo na kuchukua hatua madhubuti”.
Baada ya kauli hiyo Spika wa bunge
Mhe. Anne Makinda alikazia akitaka majibu juu ya picha za juzi
zilizosambaa zikimuonyesha Mhe. Komba akiwa na binti mdogo ambazo
mwenyewe alisema si zake na wabunge kuonekana wakitaka majibu ambapo
Mhe. Mbarawa anasema.
“Mhe. Spika kuhusu picha za juzi
zilizosambaa mitandaoni tunazifuatilia kujua zimeanzia wapi na taarifa
zake zikoje kwani hata mimi bado sijaziona ila tutachukua hatua
tutakapobaini zilipotoka
chanzo:gurudumu la habari
0 comments: