MAPENZI mmmmmh...! FAHAMU KAMA NI WAKO AU WA WENGINE
NDUGU zangu ni vizuri unaposoma makala haya kama una swali ukapiga simu badala yakuchukua maamuzi. Makala haya yanaandikwa kutokana na tafiti mbalimbali za ndani na nje ya Tanzania, kwani huwa ninashirikiana na wataalam wengine wa nje kufikia muafaka. Naandika kitaalam, na ni baada ya utafiti, hivyo ni vizuri kuchukulia ninachokiandika kama kilivyo, hata kama kinauma au kitamu. Kwa kifupi ni kwambakujua kama fulani ana wengine au la, ni kuangalia namna ambavyo anakuwa wazi kwako. Je, uliyenaye ni muwazi kwa kiasigani kwako?Ni uwazi wa namna gani ninaouzungumzia? Ni hasa katikasuala zima la mawasiliano. Ukiwana mtu halafu simu yake inakuwashida kuishika, au ukiishika anauliza ya nini? Hesabu umeumia.
Yeyote ambaye ana masharti katika simu yake ya mkononi, jua kwa asilimia kubwa si muaminifu. Unaweza kumdanganya mpenzi wako kwanamna unavyojua, lakini huu ni ukweli kwamba ukiona mtu hanaamani na simu yake huyo kwa asilimia kubwa si muaminifu.
Hakuna kazi ambayo unaweza kuifanya ikiwa ni ya siri sana kiasi kwamba hata mkeo au mumeo asijue. Hata kama ni usalama wa taifa, kabla ya kuoa ipo fomu ambayo mwanamke anapaswa kuijaza na anapaswa kufahamu mumewe au mkewe nimtu mwenye kufanya kazi gani.
Najua iko kazi moja ambayo ndiyo pekee wakati mwingine inakuwa huruhisiwi kabisa kuoa,lakini kwa mtu yeyote ambaye yuko kwenye ndoa na anasema ana mambo ya siri hawezi kumueleza mkewe au mumewe, kwa asilimia kubwa ni kudanganyana.KUTOKA NJE HAKUMAANISHI HAKUPENDI; Tafiti zinabainisha kuwa wanaume au wanawake wanaotoka nje si kwa sababu hawazipendi ndoa zao au kwamba wako tayari kwa talaka. Bali wengine wanatoka nje kwa sababu tu ya kero ndani ya nyumba kwa hiyo wanakwenda nje wakiamini watapata amani, au wengine ni kwa sababu ya umaskini, wanakwenda huko wakiamini watapata hiki na kile ambacho wanakikosa ndani. UKWELI HALISI; Hakuna amani yoyote ya dhati ambayo mtu anaweza kuipata anapokwenda nje, badala yake anakwenda kuchukua aibu na kujidhalilisha yeye mwenyewe. Amani ya kweli iko kwenye uhusiano uliopo, si kurukaruka na wanawake au wanaume. ZINGATIA; Ni muhimu kwa wapenzi kuangalia namna ya kuimarisha uhusiano baina yao. KUPENDWA AU KUACHWA: Elewa kwamba kupendwa au kuachwa sio sawa na daladala, kwamba unapanda hili na kuingia jingine. La hasha, hebu jithamini na kujiona kuwa una thamani. Usijikatie tamaa kwa kuona umeachwa basi ndiyo mwisho wa kupenda au kupendwa. Wakati mwingine kila kitu kina sababu zake.MKIACHANA USIKURUPUKE KWENDA KWA WENGINE; Siku zote mwisho wa penzi la zamani ni mwanzo wa penzi jipya. Unapoachwa usikurupuke kutoa maamuzi, siku zote maamuzi ya hasira huwa na majuto. Wapo wanaodiriki hata kulipa kisasi. Utulivu ndiyo njia pekee ya kujipanga upya. Nina imani baada ya utulivu ni muda muafaka wa kujithamini na kujiona bado una thamani mbele ya jamii. URAFIKI WA WATU WA JINSIA TOFAUTI UPO?; Urafiki wa kawaida kati ya watu wa jinsi mbili huwa ni wa pekee sana. Mara nyingi hawa watu watapaswa kuwa wanapenda vitu vinavyofanana au kutunzianasiri, kushauriana, kusoma, kufanya kazi pamoja nk.. wengine hata hufanyiana ukuwadi. Uhusiano wenyewe usipokuwa wa asili, hautakawia kuporomoka na hivyo kutofikia malengoEPUKA KUDANGANYWA KATIKA MAPENZI; Kuna mambo ambayo yanapaswa kushughulikiwa mapema ili kuepuka penzi la uongo. 1. Umaskini; Wengine wanaingia kwenye mapenzi kwa sababu ya kusaka kitu fedha, kwa hiyo ni muhimu kulichunguza hili kama ndio sababu ya kupendwa na uliyenaye 2. Dini/imani; Dini inaweza kuwa kikwazo cha kuoana, ni muhimu kuzungumza hili mapema. 3. Elimu; Tofauti kubwa ya elimu inaweza kuchangia uhusiano kuharibika 4. Umri; Ni ngumu sana kuishi kwa amani na upendo na mtu ambaye amekuzidi sana umri, kwa sababu mnakuwa mmetofautiana sana ufahamu wa mambo, wewe unataka muziki, yeye anaona kelele maanaameshasikia sana. Kwa ujumla mtu anaweza 'kukupenda' kwa sababu ya kipato chako, au mwingine atadanganya kwamba anaishi 'Dar' ili muwe wapenzi.. SIRI ZA ANAYEPENDA KWA DHATI: Anayependa kweli anajitoa kwa moyo wake wote, ila yule anayeigiza utamjua tu, hata kwa kuwangalia, na hata siku moja hawezi kufanya kitu ambacho hakipendi kukuridhisha. USIWE MWONGO; Uthubutu wa kusema uongo kabla hujaolewa, ujue wewe utakuwa muongo mpaka siku unaingia kaburini. Tuwe waaminifu na wawazi
0 comments: