Copy&paste:ANUSURIKA KUFA AKILETA MBEMBWE WAKATI WA KUOA.

...................

Alipanda kreni kumposa mpenzi.Yalomkuta?'Kreni' ilitumbukia ndani ya nyumba wakati ikimbeba mwanamume aliyekuwa anamposa mpenzi wake 


 
Mwanamume mmoja raia wa udachi amejikuta akikimbilia usalama wake baada ya jaribio la kutaka kumposa mpenzi wake kwa mbwembwe kwenda mrama.
Mtu huyo ambaye hakutajwa kwa jina anayeishi mjini Ijsselstein alikodisha 'kreni' au Crane na kuipanda akipanga kwamba kreni hilo imtoe chini na kumpanidhs hadi dirishani mwa mpenzi wake ambapo angemchezea wimbo na kisha kumposa.
Badala yake yaliyomkuta hakuyatarajia kabisa.Kreni hiyo ilianguka chini na kupita dirishani kwa mpenzi wake huku ikiangukia nyumba za majirani.
Mwanamume huyo alilazimika kukimbilia usalama wake na hakuna aliyejeruhiwa katika tukio hilo lililowaacha wengi wakiangua kicheko.
Kwa mujibu wa jarida la Algemeen Dagblad, mpenzi wake mwanamume huyo alimkubali na kusema yuko radhi kuolewa naye licha ya tukio hilo.
Baada ya kuongea na polisi, wawili hao walisafiri kwenda mjini Paris Ufaransa kusherehekea.
Kreni hio ilianguka tena kwa mara ya pili ilipokuwa inainuliwa na hata kuharibu zaidi nyumba za majirani. Meya wa mji huo, amezomewa na wengi baada ya eneo hilo kusemekana kutokuwa salama.
 shukrani:bbcswahili
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: