TOP 10 YA WASANII MATAJIRI BARANI AFRIKA.
(1). Youssou N’dour – Senegal
Youssou N’dour ni
msanii nguli na maarufu kutoka nchini Senegal na Africa kwa ujumla,
staili anayotumia kuimba mwanamuziki huyu inafahamika kama Mbalax ambao
ni mchanganyiko wa lugha za asili nchini Senegal ikijumuisha Rumba,
Jazi, rock pamoja na soul, kazi yake muziki imeweza kufanya aweze
kumiliki mojawapo ya majengo makubwa ya media nchini Senegal chenye
kituo cha Radio pamoja Televisheni ndani yake pia alipata nafasi ya
kuchaguliwa kuwa waziri wa Utalii na utamaduni mwaka 2012 pia alipata
dili la kurekodi wimbo wa ”La Cour des Grand” ambao ulitumika
kama National Anthem katika fainali za kombe la Dunia mnamo mwaka 1998
akishirikiana na mwanamuziki mwenzake Axelle Red.
(2). P Square – Nigeria
Hakuna asiyewafahamu Mapacha hawa
Peter na Paul Okoye wanaotamba na ngoma yao ya ”Personally” ambao
wanatokea nchini Nigeria, Mapacha hawa wanaosifika kwa kutoa shoo kali
na kabambe kazi yao ya muziki imewawezesha kupata tuzo kubwa
mbalimbali ikiwemo ile ya KORA AWARDS mwaka 2010 wakitajwa kama wasanii
bora wa mwaka na kwa sasa kiasi wanachoingiza kwa shoo moja ni dola za
kimarekani 150,000 wakiwa na mjengo mmoja nchini Marekani uliowagharimu
zaidi ya Dola Milioni 3 za kimarekani hiyo inawafanya washike nafasi ya
pili.
(3).D’banji – Nigeria
Dapo Daniel Oyebanjo Maarufu kwa
jina la steji D’BANJI au unaweza ukamwita KOKO MASTER kutoka nchini
Nigeria ambaye alianza kusikika rasmi kwenye miaka ya 2007 alipotoka na
kibao cha Fallin In Love kilichobamba kwa kipindi kirefu katika vituo
mbalimbali vya media huku akimshirikisha mwanama ‘Geneviv Nnaji’ ambaye
ni muigizaji nyota wa filamu Nigeria katika video ya wimbo wake huo,
D’BANJI ndiye mwanamuziki wa kwanza kutoka barani Africa kujiunga katika
rekodi kubwa ya muziki duniani ya GOOD MUSIC inayomilikiwa na Rapa
Kanye West huku akiwa amechukua tuzo za kutosha kupitia kazi yake ya
sanaa, Baadhi ya vitega uchumi alivyonavyo mwanamuziki huyo kupitia
muziki ni pamoja na Klabu ya usiku anayomiliki iliyopo nchini Nigeria,
Brand yake ya maji inayofahamika kwa jina la KOKO WATER na Reality Show
yake ya KOKO MANSION pia ni kati ya wasanii wanaoingiza mpunga mrefu
katika shoo zao.
(4).Koffi Olomide – DR Congo
(5).Salif Keita – Mali
(6).Fally Ipupa – DR Congo
(7). 2 Face Idibia – Nigeria
(8). Hugh Masekela – South Africa
(9). Banky W – Nigeria.
(10). Jose Chameleone – Uganda( East Africa).
Na larrybway

0 comments: