GARI YA MZIGO YAPATA AJALI TUNDUMA
Lori la mizigo lenye namba T120 BRA limepata ajali leo maeneo ya Anglikan Tunduma. Ajali hii ilitokea baada ya lori hilo kumgonga mtoto mmoja mwanafunzi maeneo ya Transifoma katika mji wa Tunduma. Baada ya tukio ndipo lori hilo likaporomoka kwa kasi na kumgonga mtoto wa pili na lenyewe kuangukia katika mtaro. Baada ya tukio wanausalama walifika eneo la tukio kwaajili ya kutoa huduma ya ulinzi wa gari na mzigo, Lakini Dreva wa gari na msaidizi wake hatukuweza kujua wapo wapi hadi tunatoa habari hii.
0 comments: