MEZ B AFARIKI DUNIA
Msanii Mez B aka Moses aliyekuwa Mkoani Dodoma kwa matibabu baada ya
kurudishwa nyumbani na mama yake amefariki Dunia. Mez B alikuwa
akiuguliwa na homa ya mapafu [TB] na alikuwa kwenye dozi na leo ilikuwa
siku ya tatu toka anatumia dawa hizo.
Leo asubuhi aliamka na kunywa dawa na chakula ila hali yake haikuwa sawa
na kuonekana amelegea. Daktari wake alipigiwa siku na kuamuru awekewe
drip ila hali yake ikawa mbaya zaidi, wakati wanampeleka hospitalini
alifia walipofika mapokezi. Jirana amelezea haya.
Pole kwa familia ya Mez B, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema, Amen.
chanzo:E S media
O
0 comments: