Ommy Dimpoz aishia kunusa airport tu na kurudi na kurudi bongo, arudishwa Bongo na ndege iliyofata..wapi huko soma hapa

...................

Safari ya Ommy Dimpoz kuelekea Vegas, Marekani kwa ajili ya kupiga show imeishia airport ya marekani, baada y akuzuiliwa kuingia Marekani na kurudishwa na ndege inayofata.
Habari zilizotufikia ni kuwa Dimpoz amerudishwa na kukataliwa kuingia ndani ya Marekani kwa kushindwa kufata msharti ya visa, ambapo visa aliyosafiria ilikuwa sio visa inayomruhusu kufanya show, na hivyo kumtilia shaka.


baada ya kuongea na meneja wake Mubenga amesema, yeye mwenyewe hajui kinachoendelea na alijaribu kumtafuta bila mafanikio na sio kawaida ya Ommy kutokumjulisha kama amefika katika safari zake.

" tangia tulivyoachana ile ijumaa nilivyompeleka airport, hatujawasiliana mpaka leo asubuhi ndio amenitumia meseji, kwasababu mi mwenyewe nilikuwa namtafuta simpati, kwahiyo na mi mwenyewe nilikuwa na wasiwasi sababu sio kawaida yake, siku zote waga akisafiri anapofika tu lazima aniambie kwamba amefika salama sasa safari hii nimeona kimya......
Ila leo asubuhi kwenye majira ya saa tatu amenicheki kuwa yupo njiani anarudi, anaingia leo usiku kwahiyo mpaka kesho mtakuwa na majibu, hajanieleza kwanini, aaaah mi nnachojua yeye anavisa ya marekani ya mwaka mmoja ya kufanya kazi" amesema Mubenga
chanzo:mbonde blog
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: