SAA 10:47 AM KINACHOENDELEA TUNDUMA KUHUSIANA NA MAANDAMANO YA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI
Mkuu wa wilaya na uongozi wa wilaya na halmashauri ya mji mdogo walifika na kuzungumza na wanachi wa Tunduma.Uongozi uliwataarifu wananchi kuwa watu wa ujenzi wa barabara wapo njiani kuja Tunduma kwaajili kujenga matuta ili kupunguza ajali barabarani.
Diwani aliwaomba wanachi wawe na subira juu ya jambo hili lakini kama serikali hawatatekeleza basi wananchi watarudi tena kushinikiza
Mhe:Diwani aliomba serikali ihakikishe katikati ya mji wa Tunduma pasiwepo na parking ya magari ya mizigo,badala yake perking zote ziwe kuanzia eneo la chapwa kuelekea mbeya. Taarifa zaidi tutaendelea kuwajulisha kadili muda unavyozidi kwenda
0 comments: