JUMA NATURE NA WENZAKE KUITEKA DAR ES SALAAM KATIKA TAMASHA LA KOMAA LITAKALOFANYIKA JUMAMOSI UKUMBI WA DAR LIVE MBAGALA ~ HABARIKA BLOG

...................
JUMA NATURE NA WENZAKE KUITEKA DAR ES SALAAM KATIKA TAMASHA LA KOMAA LITAKALOFANYIKA JUMAMOSI UKUMBI WA DAR LIVE MBAGALA ~ HABARIKA BLOG

Msanii
Juma Nature 'Kiroboto' akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu tamasha kubwa la kuadhimisha
miaka 16 ya kazi zake za muziki nchini  pamoja na hitimisho la sherehe
za mwaka mmoja za Kituo cha Redio cha EFM linalofahamika kwa jina la
Komaa Concert litakalofanyika kwa mara ya kwanza Jumamosi Ukumbi wa Dar
Live Mbagala kuanzia saa 12 jioni. Kushoto ni  Mkurugenzi wa Idara ya
Mahusiano na Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis Ssebo, ambao
ni waandaaji wa tamasha hilo. Kulia ni Meneja wa Maendeleo ya Biashara
wa Kampuni ya Microphas Insurance Agency Ltd, Mansoor Kipolelo wa
dhamini wa tamasha hilo.
Mkurugenzi
wa Idara ya Mahusiano na Mawasiliano wa Kituo cha Redio cha EFM, Denis
Ssebo (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Msanii
Said Christopher 'Mucky), Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa Kampuni ya
Microphas Insurance Agency Ltd, Mansoor Kipolelo wa dhamini wa tamasha
hilo,Msanii  Juma Nature, Msanii, Semani Jabiri 'Msagasumu' na Msanii
Snura Mushi.
Wasanii
watakaotoa burudani la nguvu siku hiyo ya tamasha. Kutoka kulia, Fredy
Felix 'Fredwayne' Juma Nature, Snura Mushia, na Said Christopher 'Mucky)


Ofisa Habari wa Kituo cha Redio cha EFM, Lydia Moyo (kushoto), akiperuzi simu yake katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua tukio hilo.

............................................................................................................
                              TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
                                              KOMAA CONCERT

Tamasha
kubwa la kuadhimisha miaka kumi na sita ya msanii JUMA NATURE  maarufu
kama kiroboto pamoja na hitimisho la sherehe za mwaka mmoja za 93.7 EFM linalofahamika
kama KOMAA CONCERT kwa mara ya kwanza litafanyika rasmi  jumamosi hii
ya  tarehe 30 mwezi mei katika ukumbi wa Dar Alive –Mbagala,  kuanzia
saa kumi na mbili jioni.

Tamasha
hili limeandaliwa na Juma nature akishirikiana na EFM kwa lengo la
kuwaburudisha Mashabiki wa juma nature na wasikiliazaji wa 93.7 EFM
ikiwa ni sehemu ya kuwashukuru mashabiki kwa ushirikiano wao kwa miaka
kumi na sita ya muziki tangu kuanza msanii huyo  Juma Nature aingie
kwenye game ya Muziki nchini Tanzania.

Aidha,
mashabiki watapata burudani kutoka kwa kiroboto  ambaye atatumia dakika
180 akiwa jukwaani kuhakikisha anakonga nyoyo za mashabiki wake ambapo
ataimba nyimbo zake zote kali zilizofanya vizuri na kusindikizwa na
wasanii kibao.

Miongoni mwa wasanii hao ni pamoja na  Profesa Jay, Shetta, Snura, Makomando, Msagasumu na wengine wengi.

Tunatoa
wito kwa mashabiki wote wa juma nature , Efm Radio, wadau na wengine
kujitokeza kwa wingi siku ya tamasha hili ili kupata burudani hii ya
kihistoria ambapo kiingilio kitakuwa ni shilingi 7,000 tu.

Tunaamini
Juma nature ni msanii mwenye kipaji kikubwa na aliyewahamasisha wasanii
kibao kuingia katika muziki huu wa kizazi kipya hivyo anastahili kupewa
heshima kubwa kwa mchango wake mkubwa katika kukuza muziki wa kizazi
kipya.

Lakini kwa Efm huyu ni msanii wa Kwanza itaendelea kufanya hivyo kwa wasanii wengine kwakuwa kwetu sisi tunaamini Muziki unaongea. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: