Masikini yaliyomkuta mtoto wa Pele....
Mwanawe Pele jela miaka 33
Mwanawe gwiji wa soka Brazil na
duniani kote, Pele, Edinho Pele, amefungwa jela miaka 33 kwa kufanya
biashara haramu ya pesa au kujipatia pesa chafu zilizotokana na biashara
ya ulanguzi wa dawa za kulevya.
Edinho ni mchezaji soka mstaafu, aliyecheza kama
mlinda lango katika klabu ya Santon aliyowahi kuchezea Pele mapema
miaka ya tisini.Edinhio, alikiri kosa la kuwa mraibu wa dawa za kulevya lakini alikanusha madai ya kuhusika na ulanguzi wa dawa hizo.
Uamuzi wa mahakama ulitolewa mjini Praia Grande, katika jimbo la Sao Paulo.
Vyombo vya habari nchini humo bado havijaweza kupata kunena na Edinho, ambaye jina lake halisi ni Edson Cholbi do Nascimento, lakini vinasema kuwa huenda akakata rufaa.
Pele, au kwa jina lengine, Edson Arantes do Nascimento, alisakatia soka yake nchini Brazil , na kuwakilisha Brazil katika kombe la dunia mwaka 1958, 1962 na 1970 na kupata sifa ya kuwa mchezaji bora katika kizazi chake.
Pele mwenye umri wa miaka 73, alishinda kombe la dunia mara tatu akichezea Brazil na kuingiza zaidi ya mabao 1,200 katika historia yake ya kucheza.
Alistaafu mwaka 1974, lakini akaanza kucheza tena mwaka mmoja baadaye mjini New York Marekani.
Edinho ni mtoto wa tatu wa Pele kutoka kwa ndoa yake ya kwanza
chanzo:bbcswahili
0 comments: