Majanga:Benki za Ugiriki kufungwa.
Waziri mkuu wa
Ugiriki Alexis Tsipras amesema Jumapili kuwa benki za nchi hiyo huenda
zitafungwa na utoaji wa fedha taslimu ukawekewa masharti.
Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras amesema Jumapili kuwa benki
za nchi hiyo huenda zitafungwa na utoaji wa fedha taslimu utawekewa
masharti kutokana na mzozo kuhusu deni kati ya Athens na wakopeshaji wa
kimataifa kutopata suluhisho. Katika taarifa aliyoitoa kwenye
televisheni ya taifa, Bw Tsipras amelaumu wakopeshaji kwa mzozo huo
ambao unatishia Ugiriki kuondolewa kwenye uanachama wa mataifa 19
yanayotumia sarafu ya Euro. Hata hivyo hakubainisha ni muda gani ambao
benki za Ugiriki zitafungwa wala athari za udhibiti wa mitaji. Muda wa
kupatiwa msaada wa kifedha unakwisha Jumanne wakati Ugiriki inataka
isaidiwe dola bilioni 8 zaidi ili iweze kulipa deni la dola bilioni 1.8
kwa shirika la kimataifa la fedha IMF. Lakini Athens inasita kutekeleza
masharti yaliyotolewa na wakopeshaji ya kubana matumizi ikiwa ni
pamoja na makato zaidi ya malipo ya uzeeni. Benki kuu ya Ulaya imesema
kuwa imeweka fedha za dharura kwa benki za Ugiriki wazi wakati kukiwa na
misururu mirefu kwenye mashini za kutolea pesa, watu wakijaribu kutoa
fedha walizoweka kwenye mabenki.
chanzo:VOA
chanzo:VOA
0 comments: