HAYA SASA HII NDO SIASA, FUATILIA YALIYOJIRI KWA LOWASA JUU YA MAAMUZI YAKE YA KUHAMA CHAMA, NA NINI KASEMA WAKATI AKIPEWA KADI YA CHAMA KIPYA

...................

Waziri  mkuu wa  zamani  Edward  Lowassa  ametangaza  rasmi  kukihama  chama  cha  mapinduzi, CCM mchana  huu  na  kutangaza  kuhamia  CHADEMA.....

 Lowassa  ametoa  kauli hii Bahari  Beach , Dar akiwa  sambamba  na  viongozi  mbalimbali  wa  UKAWA   ambao  wamekutana  na  waandishi  wa habari  kuzungumzia  hatima  yake  kuelekea  ikulu  pamoja  na  mapungufu  yaliyojitokeza  wakati  wa  mchakato  wa  kumpata  mgombea  urais  wa  CCM.

Lowassa  amesema  baada ya  kutafakari  kwa  kina  na  kujiridhisha, ameamua  kujiondoa  CCM kwa  kuwa  siyo  baba  yake  wala  mama  yake  na  kuitikia  wito  wa  UKAWA  kupitia  CHADEMA.


 Amesema  safari  yake  haitafanikiwa  iwapo  hawatajitokeza  watu  wengi  kupiga  kura na  anaiomba  tume  ya  uchaguzi  iongeze  muda  ili  watu  wote  waweze  kujiandikisha

Lowassa  amesema  alinyimwa  haki  yake  na  CCM  kama  mtanzania  kujieleza  na  kujitetea, hivyo  atakuwa  mnafiki  akisema  anaimani  na  chama  hicho.
 Baada  ya  maelezo  hayo; Mwenyekiti  wa  CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe alisimama  na  kumkabidhi  rasmi  Lowassa  Kadi  ya  CHADEMA.

1.Nimetumia wiki mbili kutafakari hatma yangu ktk Siasa, najua wengi wamesubiri kwa hamu.

2.Watu wangu wamesema fanya maamuzi magumu.. Namshukuru Mke wangu na familia wamekuwa na mimi ktk kipindi kigumu-

3.Nawashukuru watu wengi waliojitokeza kuniunga mkono wakati natafuta wadhamini-

4.Uchaguzi wa Mgombea CCM ulijaa chuki dhidi yangu, Kamati ya Maadili haikutakiwa kuchagua Mgombea-

5.Kilichotokea Dodoma kinaitwa 'kubaka Demokrasia'

6.CCM iliwatumia vijana wachache kunikashifu na baadae wakapewa Madaraka makubwa

7.Kibaya zaidi kilikuwa kuwanyima Wagombea 38 wa CCM haki ya kujieleza mbele ya Kamati Kuu

8.Nilinyimwa haki ya Msingi ya kusikilizwa na kujieleza CCM, nitakuwa mnafki kusema nina imani na CCM

9.CCM niliyoiona Dodoma sio CCM iliyonilea Kisiasa, mimi km Mtanzania mwenye Uhuru nasema sasa basi

10.Mwalimu NYERERE alisema CCM sio baba yangu wala mama yangu,nimeamua kuanzia leo naondoka CCM na kujiunga CHADEMA

11.Namshukuru sana James MBATIA na Viongozi wa UKAWA kwa kuniamini na kunipokea

 12.Naamini UKAWA tutaondoa mfumo wa Utawala wa Chama kimoja, naomba Watz wajiunge nasi ktk SAFARI YA MATUMAINI

13.Naomba Watz wajiandikishe ktk Daftari la Kupiga Kura,watunze Shahada za kupigia Kura ili tuiondoe CCM Madarakani

14.Mimi nauchukia UMASKINI, Kiongozi kujionesha maskini ni upuuzi. Natamani Watz wawe Matajiri km MENGI na AZAM

15.Kulipa kisasi ni upuuzi, umefanya nini mpaka useme nitalipa kisasi? Waulizeni wamefanya nini nilipe kisasi?

16.Kulipa kisasi ni upuuzi, umefanya nini mpaka useme nitalipa kisasi? Waulizeni wamefanya nini nilipe kisasi?

17.Msiwatishe, kama wamefanya madhambi yao waambieni nimewasamehe mimi sitalipa kisasi

18.LIPUMBA- 'UKAWA tumekubaliana maliasili na Rasilimali zitumike kwa manufaa ya Watz wote'

19.MBOWE- 'CCM imekuwa na Wabunge wengi ndani ya Bunge, imefanya waangalie maslahi yao zaidi kuliko Taifa

20.MBOWE- 'Tumekubaliana Wabunge wa UKAWA wakiingia Bungeni November 2015 waangalie zaidi maslahi wa Watz'

21.MBATIA- 'Tunawakikishia Watz kwamba nguvu kubwa ya Serikali ya UKAWA itaangalia maslahi ya Watz'

22.Nilisema mtu ambaye ana ushahidi wowote kuhusu mimi kuhusika na RICHMOND peleka Mahakamani, kama huna kaa kimya

23.Tulikuwa na tatizo la Umeme, tukahangaika kuleta Mitambo ya kuzalisha umeme.

24.Tulipata taarifa kuwa mtu ambaye tunampa kazi ya kuzalisha umeme hakuwa na uwezo

25.Niliondoka Madarakani lakini tatizo limeongezeka, mikono yangu ni misafi mwenye Ushahidi peleka Mahakamani

26.MAKAIDI- 'Nashukuru mmetuletea kifaa LOWASSA, nilimfahamu LOWASSA kupitia mtoto wangu

27.MAKAIDI- 'LOWASSA amekuja UKAWA afuate na Sisi tunavyotaka asahau kidogo mambo ya CCM'

28.MAKAIDI- 'Watanzania wamekwama, najua LOWASSA amekuja UKAWA kutukwamua.. Karibu sana LOWASSA'

29.Salum MWALIMU- 'Kuna taarifa kuwa sehemu kubwa ya Mikoa ya Mbeya, Singida na Arusha umeme umekatwa'

30.MBATIA-'Siku ya leo nina amani kutoka sakafu ya moyo wangu, ninawahakikishia Watz kuwa TZ bila CCM inawezekana'

31.MBATIA- 'UKAWA hatutamwaga damu lakini walio Madarakani wasituchokoze, uwezo wa kupambana kwa hoja tunao'

32.MBOWE- 'Tunapenda kumkaribisha LOWASSA pamoja na familia, marafiki zako na kundi la Watz wapenda haki'

33.MBOWE- 'Ujio wako CHADEMA umezua hofu nyingi kwa sababu hii ni nchi ya hofu'

34.MBOWE- 'Watu wengi wa CCM wamenipigia simu wakasema kumkaribisha LOWASSA ni kuharibu Chama'

35.MBOWE- 'Niliwajibu ni kweli ataharibu Chama, lakini nikajiuliza lini CCM ikawatakia mema CHADEMA?'

36.MBOWE- 'Kumleta LOWASSA kwenye meza hii haikuwa kitu chepesi, tumekaa Vikao viingi usiku na mchana'

37.MBOWE- 'Naongea kwa ujasiri,hatuwezi kufikiri mambo mema mapya kama tutaendelea kufikiri mambo mabaya ya zamani'

38.MBOWE- 'Chama cha Siasa ni watu, mimi niletewe watu Milioni niwakatae mimi ni mwendawazimu?'

39.MBOWE- 'Mimi na Viongozi wa UKAWA hatufikirii kulipiza kisasi'

40.MBOWE- 'Tumeshuhudia Vita ya makundi ndani ya CCM na wengine wakaadhibiwa. Wengi wanalalamika, wanaona ukweli lakini hawana uhuru kuongea'

41.MBOWE- 'Tumeshuhudia Vita ya makundi ndani ya CCM na wengine wakaadhibiwa. Wengi wanalalamika, wanaona ukweli lakini hawana uhuru kuongea'

42.MBOWE- 'Hatujamkaribisha LOWASSA pekeyake, tumemkaribisha na Mamilioni ya Watanzania

43.MBOWE- 'Chama cha Siasa ni watu, mimi niletewe watu Milioni niwakatae mimi ni mwendawazimu?'

44. MBOWE- 'Mimi na Viongozi wa UKAWA hatufikirii kulipiza kisasi'

45.MBOWE- 'Umesaidia kumfungua kifungoni Mbunge Ole MEDEYE na Wabunge wengi ambao tutaendelea kuwakaribisha'

46.MBOWE- 'CHADEMA haiongozwi kwa kauli za MBOWE, inaongozwa kwa Katiba na Kanuni za Chama

47. MBOWE- 'Namshukuru sana Rais JK, umesaidia kutujenga Upinzani kuelekea Uchaguzi wa mwaka huu'
48.MBOWE- 'LOWASSA ujitahidi sana Mazoezi kwa sababu huku kuna mabomu'
49.MBOWE- 'LOWASSA alipokuwa analalamika Dodoma sisi tulikuwa tunafurahi'
50. MBOWE- 'Umesaidia kumfungua kifungoni Mbunge Ole MEDEYE na Wabunge wengi ambao tutaendelea kuwakaribisha
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: