Yanga itafika fainali Kagame, ajigamba Pluijm
Yanga imemaliza nafasi ya pili kwenye kundi lake la A
lililokuwa na timu tano na Jumatano itacheza na ndugu zao Azam ukiwa ni
mchezo wa robo fainali
KOCHA wa Yanga Hans van der Pluijm amesema anauhakika kikosi chake
kitacheza fainali ya michuano ya Kombe la Kagame inayoendelea Jijini Dar
es Salaam.Pluijm ameiambia Goal ushindi wa bao 1-0 walioupata jioni ya leo dhidi ya Khartoum ya Sudan umedhihirisha ubora waliokuwa nao licha ya kuanza vibaya michuano hiyo kwa kufungwa na Gor Mahia kwenye mchezo wa ufungzi.
“Nafurahi kuona tumeanza kurudi kwenye ubora wetu baada ya kuanza vibaya kila mchezo tumekuwa tukibadilika na kiwango tulichokionyesha leo ni tofauti kabisa na kile tulichoonyesha kwenye mechi zetu tatu zilizopota na hii ni ishara kwamba tunataka ubingwa,’amesema Pluijm.
Yanga imemaliza nafasi ya pili kwenye kundi lake la A lililokuwa na timu tano na Jumatano itacheza na ndugu zao Azam ukiwa ni mchezo war obo fainali.
chanzo:goal.com
0 comments: