MBASHA YAMKUTA YA KUMKUTA JUU YA KESI YAKE YA UBAKAJI.....SOMA HAPA
MAHAKAMA
ya Wilaya ya Ilala imesema mfanyabiashara na muimbaji wa muziki wa
injili Emmanuel Mbasha ana kesi ya kujibu katika shtaka linalomkabili la
ubakaji linalomkabili.
Katika shtaka hilo Mbasha anadaiwa kumbaka binti mwenye umri wa miaka 17 (jina linahifadhiwa) ambaye ni shemeji yake.
Mbele
ya Hakimu Flora Mjaya, mwendesha Mashtaka Munde Kalombola alidai
mahakama imemkuta Mbasha na hatia baada ya kupitia ushahidi wa pande
zote mbili.
Mbasha
ambaye ni mume wa muimbaji maarufu wa muziki wa injili Flora Mbasha
anadaiwa kumbaka shemeji yake huyo kati ya Mei 23 na 25 mwaka huu eneo
la Tabata ambako alikuwa akiishi naye.
Kesi
hiyo ilianza kusikilizwa mahakamani hapo Septemba 5, 2013 ambapo binti
huyo aliieleza Mahakama kuwa alibakwa na shemeji yake (Mbasha) kwa awamu
mbili tofauti kabla ya kufanikiwa kukimbia.
Kwa
mujibu wa Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya mwaka 2003 sura ya
20 kifungu cha 186, kifungu kidogo cha tatu, kesi hiyo inasikilizwa na
Mahakama ya siri ili kulinda haki ya binti huyo.
Kesi
hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Julai 23, mwaka huu ambapo Mbasha
anatakiwa kufika na mawakili wake ili kujitetea dhidi ya shtaka hilo.
0 comments: