SOMA JINSI GANI MAGUFULI KAANDALIWA KUWA RAIS

...................


Leo katika pitapita zangu za kumsoma wa sifu wa Rais wetu mtarajiwa Dr John P. Magufuli niligundua ana sifa za pekee na tayari Serikali ilikuwa imeshamuandaa kisaikolojia ili aje awe Rais akimaliza Dr Jakaya M. Kikwete.

Kwa nini nimesema hivo.
1)Ni nadra sana kwa kiongozi wa serikali asiekuwa Rais kuitumia Ndege ya serikali hata kwa shida yoyote.sasa ni kwa nini Magufuli alitunikiwa ndege amsafirishie maiti ya mtoto wake,jee hakukuwa na ndege nyingine za kusafirishia. 

2)Kwanini wakati wa kutangaza nia Magufuli alikuwa mpole sana na hakufanya kampeni hata kidogo,tofauti na wenzake waliohukumiwa na Tume ya Maadili ya CCM.


3)Kwanini msafara wa Magufuli akiwa ni Waziri tu,ulikuwa unapewa ulinzi mkubwa kuliko Mawaziri wenggine.

4)Kwanini Kikwete wakati wa Uongozi wake alikuwa anamsifu sana Magufuli kuliko Mawaziri wengine, au tuseme alimpa ujenzi wa Barabara ili ije iwe ndio kampeni ya 2015, Kwamba CCM imejenga Barabara Mijini na Vijijini, na aliesimamia Ujenzi huo ni huyo Rais anaewaomba Kura.

Kwa vyovyote vile naipongeza Intelijensia ya Ikulu ili uwe Rais ni lazima wawe wamukuandaa wao,na sio ukurupuke tu.

Hongera Rais Pombe Magufuli ingawa jina lako halisaound vizuri kwa cheo cha Urais,ila una akili na nina imani nawe kuwa utakuwa Rais Bora.

Ombi langu kwako.
Punguza ukali wakati mwengine, ni vyema ukawa kama mtangulizi wako Kikwete,yaani wakati wa serious uwe serious na muda mwengine uwe mwelewa,ukishauriwa na wenzako uwe mtaratibu2


chanzo :specialsweetnesstz255.blogspot.ae
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: