MGAMBO MWISHO KUKAMATA WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO - CCM
Baadhi ya wanachama wa CCM wakimkabidhi zawadi katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu.
Anjela Kairuki mmoja wa wajumbe wa kamati ya kampeni ya taifa akizungumza katika mkutano wa mgombea mwenza.
Na Joachim Mushi, Arusha
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kikifanikiwa kushinda Uchaguzi Mkuu wa
Oktoba kitahakikisha mgambo wa halmashauri ya jiji hawawasumbui kwa
kamatakamata za wafanyabiashara ndogondogo ambao wengi wao ni akinamama
pamoja na vijana.
Kauli
hiyo imetolewa leo na mgombea mwenza nafasi ya urais tiketi ya CCM, Bi.
Samia Suluhu alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara katika mkutano
uliofanyika uwanja wa Kilombero Jimbo la Arusha Mjini na kuhudhuriwa na
umati wa wana CCM na wananchi wengine.
Akinadi
ilani ya CCM alisema chama hicho kimeandaa utaratibu mzuri wa fursa kwa
akinamama na vijana wanaofanya biashara ndogondogo hivyo itakuwa ni
marufuku kwa mgambo wa jiji kukamata biashara za akinamama na vijana
wanaojitafutia ridhiki mjini.
"Iwapo
CCM itafanikiwa kuingia mjini naomba wale mgambo ambao uishi kwa
kutegemea kukamata kamata bidhaa za akinamama watafute kazi nyingine ya
kufanyanya...hatutaki mgambo wa kufanya kazi hizo ni marufuku," alisema mgombea huyo mwenza wa CCM, Samia Suluhu.
Alisema
Ilani ya CCM imepanga kujenga viwanda vya kuchakata madini ili
kuhakikisha vijana wanapata ajira na kuweza kukuza vipato vyao, na
kufufua viwanda vilivyosimama kikiwemo cha 'General Tyre' ikiwa ni
mpango wa kumaliza tatizo la ajira kwa vijana.
Aidha
alisema mpango mwingine ambao upo kwenye ilani ya CCM ni kushughulikia
tatizo la mikataba ya ajira ya madereva wa magari madogo na makubwa,
"Tukifanikiwa
kuingia Ikulu kazi ya kwanza tutakayoipa Wizara ya ajira ni kuhakikisha
inafanya kazi ya kushughulikia mikataba ya ajira kwa madereva wa magari
madogo na makubwa," alisema Bi. Suluhu.
Aliongeza
Serikali ya CCM itaunda ufuko wa maji kuakikisha huduma za maji
zinakuwa za uhakika kwani Mkoa wa Arusha unashughuli nyingi na idadi ya
watu inakuwa kila uchao.
Serikali
ya CCM imepanga kushughulikia suala la rushwa na vitendo vya ufisadi,
uzembe ili kuhakikisha kasi ya maendeleo inaongezeka. Awali kabla ya
mkutano wa Arusha Bi. Suluhu alifanya mikutano katika majimbo ya Hai,
Siha na Arumeru yaliyopo mikoa ya Kilimanjaro kabla ya kuingia Mkoani
Arusha.
Akiwa
katika majimbo hayo mgombea aliinadi ilani ya CCM pamoja na kuwanadi
wagombea ubunge na madiwani wa CCM wa maeneo hayo. Ambapo alisema
Serikali ya CCM imepanga kuboresha huduma za afya, elimu, uwezeshaji wa
vijana na akinamama ikiwa ni pamoja na kutenga shilingi milioni 50 kwa
kila kijiji kwa ajili ya kuwainua akinamama na vijana.
Baadhi ya wananchi na viongozi wa wafugaji wa kimasai wakifuatili kutanoBaadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia Jimbo la Arumeru.
Agrey Mwanri akizungumza na wapiga kura wakeBurudani kwa wananchi na mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara moshi Mjini.Agrey Mwanri (kushoto) akifuraiya jambo na Bi. Ummy Mwalimu (kulia) kwenye mkutano wa B, Samia Suluhu.Baadhi ya wananchi wakimsikiliza mgombea mwenza wa tiketi ya CCM akihutubia jimbo la Hai.Baadhi ya wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa katika mkutano wa hadhara wa mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu Arusha Mjini.Burudani kwa wananchi na mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara moshi Mjini.
chanzo: http://www.lindiyetu.com
0 comments: