Mourinho:Daktari'mjinga' hatakuwepo uwanjani
Meneja wa Chelsea manager Jose Mourinho amekariri msimamo wake dhidi ya kitengo cha utabibu cha timu yake.
Mourinho
aliwakaripia Dakta Eva Carneiro na Jon Fearn kwa kuingia uwanjani huku
timu hiyo ikisalia na wachezaji wachache kufuatia kufurushwa kwa kipa
nambari moja Thibaut Courtois katika mechi ngumu ya kufungua msimu kati
yao na Swansea .'The special one' alisema kuwa daktari mkuu Carneiro na msaidizi wake Fearn hawatakuwa uwanjani Chelsea itakapokuwa ikipambana na Manchester City siku ya jumapili.
Kocha huyo aliyasema hayo baada ya kukutana na kitengo kizima cha utabibu cha Chelsea siku ya Alhamisi.
Carneiro aliwakilishwa katika mkutano huo na mawakili wake kutoka kwa kampuni ya mawakili ya Mishcon de Reya.
Kutokana na shinikizo la wapinzani wao Mourinho aliona kuwa kumuondoa Hazard katika kipindi hicho kuliwasaidia wapinzani wao kuwa na wachezaji wawili zaidi hivyo kuwazidi nguvu.
''Mimi nao tunahusiana kama kawaida tu vile ''
''Walinieleza kuwa wanahitaji kukosolewa ili na wao wajiendeleze''
chanzo:bbcswahili

0 comments: