Wahubiri wa TZ waliotekwa kuwachiliwa
Mtu
anayeongoza mazungumzo ya kuachiliwa huru kwa wahubiri saba wa kiislamu
kutoka Tanzania waliotekwa nyara wiki iliopita ameiambia BBC kwamba
makubaliano ya kuwaachilia huru huenda yakaafikiwa hivi karibuni.
Sheikh
Suleiman Mohammed amesema kuwa kundi la watu wanaofanya mazungumzo hayo
limewasiliana na watekaji nyara hao na kwamba viongozi hao wa dini
hawajateswa.''Wametaka kupewa fedha ili kuwahudumia mateka hao iwapo fedha za fidia hazitalipwa'',aliambia BBCswahili.
Ameongezea kuwa maimamu hao sio waliokuwa wakilengwa na washambuliaji hao na kwamba walikuwa katika mahala pabaya katika wakati usiofaa
chanzo:bbcswahili
0 comments: