Kikosi cha Taifa Stars Chatajwa,kingia kambini kesho
Morocco amesema kikosi kitaingia kambini Octoba 1 tayari kuanza mazoezi ya kujiwinda na mechi hiyo itakayopigwa Octoba 7
KOCHA msaidizi wa timu ya taifa ya Tanzania ‘TaifaStars’ Hemed
Morocco ametangaza majina ya wachezaji watakaoingia kambini kujiandaa na
mechi dhidi ya Malawi kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia
mwaka 2018 nchini Urusi.Morocco amesema kikosi kitaingia kambini Octoba 1 tayari kuanza mazoezi ya kujiwinda na mechi hiyo itakayopigwa Octoba 7 mwaka huu kwenye uwanja wa taifa Stars ikiwa mwenyeji wa mchezo huo.
Walioitwa kwenye timu ya taifa kujiandaa na mchezo wa Malawi ni.
Magolikipa:
Ally Mustafa (Yanga), Aishi Manula (Azam FC) Said Mohamed (Mtibwa Sugar)
Mabeki:
Shomari Kapombe (Azam FC), Mohamed Hussein, Hassan Isihaka (Simba), Juma Abdul, Haji Mwinyi, Kelvin Yondani, Nadir Haroub (Yanga)
Viungo:
Himid Mao, Mudathir Yahya, Frank Domayo, Farid Mussa (Azam FC) Salum Telela, Deus Kaseke Simon Msuva (Yanga), Said Ndemla (Simba)
Washambuliaji:
John Bocco (Azam FC), Rashid Mandawa (Mwadui FC), Ibrahim Ajib (Simba), Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe-Congo DRC), Mrisho Ngassa (Free State Stars-Afrika Kusini).
chanzo:goal.com
0 comments: