KUTOKA BBCSWAHILI:Washukiwa 38 wa ugaidi wakamatwa TZ
Polisi nchini
Tanzania wanasema wamewakamata washukiwa 38 wa ugaidi ambao wanauhusiano
na kundi la kigaidi lililofanya mashambulio katika vituo kadhaa vya
polisi nchini humo.
Washukiwa hao walikamatwa wakiwa na bunduki
kumi na risasi 387, mabomu ya kurushwa kwa mkono maarufu kama grunedi na
vifaa vya kutengenezea mabomu.
Hata hivyo idara ya polisi nchini Tanzania, halijasema ni lini washukiwa hao walikamatwa au siku watakayofikishwa mahakamani.
Katika
kikao na waandishi wa habari, mkuu wa polisi Suileman Kova,
aliwaonyesha waandishi wa habari silaha walizonasa kutoka kwa washukiwa
hao.
Amesema uchunguzi wa awali, umebainisha kuwa kuna uwezekano mkuwa kuwa waliokamatwa wana mitandao mingine ya kigaidi.
Amesema washukiwa hao walikamatwa baada ya operesheni kali iliyofanywa katika miji ya Lindi na Tanga.
Bila kutaja majina yao, Kova amesema kuwa miongoni mwa wa waliokama ni wavulana walio na umri wa chini ya miaka 17.
Kukamatwa
kwa washukiwa hao kunajiri baada ya vituo vinne vya polisi kushambuliwa
nchini Tanzania, tukio la hivi karibuni likiwa shambulio dhidi ya kituo
cha Staki Shari mjini Dar e Salaam.
Julai 15, mwaka huu watu
waliokuwa wamejihami walishambuio kituo cha polisi mji Dar es Salaam na
kuwauawa maafisa saba wa polisi na raia kadhaa, kabla ya kutoweka na
idadi ya silaha isiyojulikana.
Katika tukio lingine lililofanana
na filamu, watu waliokuwa wamejihami walishambulia kituo cha polisi
katika wilaya ya Bukombe, eneo la Geita na kuwauawa maafisa wawili wa
polisi.
chanzo:bbcswahili
0 comments: