MWILI WA DR KIGODA KUWASILI LEO NCHINI

...................
MAREHEMU Dk Abdalala Kigoda enzi za uhai wake(Pichani) 

 Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Dk Abdalala Kigoda aliyefariki  nchini India unatarajia kuwasili leo mchana tayari kwa ajili ya mazishi.

Ofisa habari wa Bunge, Prosper Minja ameiambia Mwananchi kuwa mwili huo utawasili saa nane mchana kwa ndege ya Emirates na kwenda kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya jeshi ya Lugalo.

Minja amefafanua kuwa shughuli za kuaga mwili huo zitafanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee kuanzia saa mbili asubuhi ambapo wananchi,wabunge na viongozi mbalimbali watapata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho.

“Taratibu zote za kuaga zitafanyika Karimjee na hapo ndipo tunategemea watu wa kada mbalimbali watafika kutoa heshima zao za mwisho kwa Dk Kigoda”amesema Minja.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mussa Uledi ameeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa mazishi kufanyika siku ya Alhamisi.
“Kuna kamati maalum inayohusika na msiba nadhani ikifikia uamuzi itatoa taarifa ila ninachofahamu mazishi yatafanyika Alhamisi nyumbani kwako Handeni” amesema Uled

chanzo: http://www.matukiotz.co.tz
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: