ZIFAHAMU SABABU ZA KUFUTWA KWA MATOKEO YA UCHAGUZI ZANZIBAR
Sababu 8 za kufutwa kwa uchaguzi Zanzibar
Hizi ndizo sababu
nane zilizotolewa na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa kisiwani Zanzibar
Bw Jecha Salim Jecha kuhusu kufutiliwa mbali kwa matokeo ya uchaguzi wa
eneo hilo.
1. Makamishna wa uchaguzi katika tume hiyo walipigana kutokana na tofauti zao2. Makamishna walikuwa na upendeleo fulani.
3. Katika vituo vyengine, hususan kisiwani Pemba,ambacho ni miliki ya Zanzibar, kura zilizopigwa zilikuwa zaidi ya zilizosajiliwa.
4. Masanduku ya kupigia kura hayakupewa ulinzi wa kutosha na maajenti pamoja na maafisa wa uchaguzi.
5. Maajenti wa vyama walifukuzwa katika vituo kadhaa.
6. Vijana walivamia vituo vya kupigia kura wakiwa na lengo la kuzua ghasia.
7. Vyama vya kisiasa vimekuwa vikiingilia tume hiyo.
8.Kura ziliharibiwa hususan zile kutoka Pemba.
chanzo:bbcswahili
0 comments: