IFAHAMU HISTORIA YA KESI YA SHEIKH PONDA BAADA YA KUACHIA HURU
MAHAKAMA ya hakimu mkazi Morogoro imemuachia huru leo Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda aliyekuwa akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi baada ya mahakama kutoridhishwa na ushahidi wa upande wa mashtaka na hivyo kuonekana hana hatia.
********
Historia ya kesi ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu
Tanzania, Sheikh Issa Ponda.
Hati ya Mashitaka ya Kesi hiyo ilikuwa na jumla ya Mashitaka matatu
lakini Julai 22 mwaka 2015, Hakimu Mkazi Mary Moyo alitoa
uamuzi wa kumfutia shitaka la kwanza kwasababu lilishatolewa uamuzi na
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, na hivyo mahakama hiyo ya Morogoro siku
hiyo ilitoa uamuzi wa kumuona ana kesi ya kujibu katika mashitaka mawili
yaliyosalia ambalo ni kosa la pili na la tatu .
Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro ilimfungia dhamana Sheikh
Ponda baada ya kukubaliana na hati ya aliyekuwa Mkurugenzi wa
Mashitaka(DPP), wakati huo Dk.Eliezer Feleshi ambaye kwasasa ni Jaji wa
Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam liloomba Mahakama hiyo imfungie dhamana
mshitakiwa huyo chini ya Kifungu cha 148(4) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya
jinai ya Mwaka 2002.
Hatua hiyo ya kufunguliwa kesi katika Mkoa wa Morogoro ilikuja
ikiwa ni muda mfupi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam,
Agosti 19 Mwaka 2013 saa Tatu asubuhi, kumfutia kesi ya jinai
Na.144/2013 katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano baada ya DPP
kudai kuwa hana nia ya kuendelea kumshitaki katika kesi hiyo No.144/2013
kwa mujibu wa kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai
ya mwaka 2002.
Hata hivyo baada ya hakimu Liwa kumwachilia huru,Ponda ambaye
aliletwa mahakamani hapo saa 12 asubuhi na wanausalama wa polisi na magereza
chini ya ulinzi mkali, alikamatwa tena na kupakizwa kwenye magari ya
wanausalama hao ambapo baadhi ya wanausalama hao waliliambia gazeti hili kuwa
wanampeleka Ponda mkoani Morogoro kwaajili ya kufunguliwa makosa matatu ya
uchochezi, kufanya mkusanyiko haramu na kisha akarejeshwa gereza la Segerea Dar
es Salaam , lakini baadae Uongozi wa Jeshi la Magereza uliamua kumuamisha Ponda
kutoka Gereza la Segerea na kumuamishia Katika Gereza Moja Mkoani Morogoro.
Sheikh Ponda alifikishwa mahakamani hapo akiwa chini ya ulinzi
mkali wa polisi, baada ya kuwasili kwa helikopta ya Jeshi la Polisi katika
uwanja wa gofu mjini Morogoro.
Akisoma mashitaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa
Morogoro, Richard Kabate, Mwanasheria Kiongozi wa Serikali, Bernard
Kongola, alidai kuwa Agosti 10, mwaka 2013, katika eneo la Uwanja wa
Ndege, Manispaa ya Morogoro, Ponda aliwaambia Waislamu wasikubali uundwaji wa
kamati za ulinzi na usalama za misikiti, kwa madai kuwa zimeundwa na BAKWATA,
ambao ni vibaraka wa CCM na serikali.
Alidai kuwa Sheikh Ponda ambaye anatetewa na wakili wa
kujitegemea Juma Nassor aliwaagiza waumini hao kuwa endapo watu hao
watajitokeza kwao na kujitabulisha kwamba ni kamati za ulinzi na usalama za
misikiti, wafunge milango na madirisha wawapige.
Ilielezwa kuwa kauli hiyo ni kinyume cha agizo la Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, iliyotolewa na Hakimu Victoria Nongwa Mei 9, mwaka 2010,
ambayo ilimtaka Ponda ndani ya mwaka mzima kuhubiri amani na Kuwa Raia Mwema.
Katika shitaka la pili, Kongola alidai kuwa Agosti 10, mwaka huu,
katika eneo la Uwanja wa Ndege, Morogoro, Ponda aliwaambia Waislamu kuwa
serikali ilipeleka jeshi Mtwara kushughulikia suala la vurugu iliyotokana na
gesi ili kuwaua, kuwabaka na kuwatesa wananchi, kwa sababu asilimia 90 ya
wakazi hao ni Waislamu.
Kwamba, Ponda aliwaambia wafuasi wake kuwa serikali haikufanya
hivyo kwa wananchi wa Loliondo walipokataa Mwarabu asipatiwe kipande cha ardhi
ya uwindaji baada ya kudai ni mali yao, kwa sababu asilimia 90 ya wakazi wa
huko ni Wakristu.
Shitaka la tatu ambalo linafafana na lile la pili, ambalo nalo
linadaiwa kutendwa Agosti 10, mwaka huu, ambapo kauli ya Ponda inadaiwa kuumiza
imani za watu wengine kinyume cha kifungu cha sheria namba 390 na kanuni ya
adhabu namba 35 cha mwaka 2002.
Oktoba 18 mwaka 2012, Ponda na wenzie 49 walifikishwa Katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa Mara ya kwanza wakikabiliwa na
makosa matano, kosa la kwanza ni la kula njama, kujimilikisha mali, kuingia kwa
jinai katika kiwanja cha Chang'ombe Markas,wizi wa malighafi zenye
thamani ya Sh. Milioni 59 na kosa la uchochezi ambapo katika kesi hiyo Jamhuri
ilikuwa ikiwakilishwa na wakili Mwandamizi wa Serikali , Tumaini Kweka
.Mahakama pia iliwafunga dhamana ya Ponda na mshitakiwa wa pili tangu 0ktoba 18
Mwaka 2012 hadi siku Kesi hiyo iliyotolewa hukumu Mei 9 Mwaka 2013.
Mei 9 mwaka 2013 Hakimu Mkazi Victoria Nongwa akitoa hukumu
yake katika kesi hiyo ya Ponda na wenzake alisema anawaachiria huru washitakiwa
49 kwasababu upande wa jamhuri umeshindwa kuthibitisha kesi dhidi
yao na kwamba anamtia hatiani Ponda kwa kosa moja tu la kuingia kwa jinai
na kwamba na anamuachiria huru katika makosa manne yaliyosalia kwasababu pia
jamhuri ilishindwa kuthibitisha mashitaka hayo dhidi ya Ponda.
Sheikh Ponda alikataa rufaa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
Salaam kupinga hukumu ya Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mei 9 mwaka 2013 ambapo
alishinda rufaa yake.
Hata hivyo siku Chache baada ya Kufungwa Kifungo hicho cha nje Mei
9 mwaka 2013, Ponda alikwenda Mkoani Morogoro na kufanya mkutano ambao alidai
wa Kutenda makosa ya jinai ambao alikamtwa Agosti Mwaka 2013 na kuwekwa
chini ya ulinzi na kufunguliwa Kesi Mahakama ya Kisutu Na.144/2013 ikafutwa na
DPP na ndipo akafunguliwa kesi hiyo Mkoani Morogoro ambayo imetolewa hukumu Leo
na kuachiwa huru.
0 comments: