LEO KATIKA HISTORIA:MAPINDUZI YA ZANZIBAR YA SAA TISA
Zanzibar
ni maarufu katika historia ya vita vifupi. Vita vya karne ya 19 ambavyo
vilimalizika kwa kiasi cha dakika 45 lakini vimetumika kuonyesha mara zote
ukatili kabla ya utawala wa ukoloni wa Ulaya Afrika Mashariki.
Kitu
ambacho kinajulikana kwa uchache kabisa ni
kumbukumbu ya karne ya 20, ambapo Zanzibar ilishuhudia mfano wa vita
vifupi kabisa vya Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964. Katika Mapinduzi haya,
Serikali ilidumu zaidi ya karne ilipinduliwa si chini ya siku moja. Taifa huru
jipya la Zanzibar la jamii ya kisultani inayojumuisha waarabu, wahindi,
waswahili, wangazija na wenyeji ikiongozwa na mrithi wa Sultani lilipotea kwa
haraka ya ajabu.
Usiku
huo ulitawaliwa na hali ya wasiwasi, kushangaza, ushupavu na kukata tamaa.
Usiku huo ulianza saa tisa usiku. Kabla ya siku kuu kubwa ya kidini . Siku kuu
hii iliwashajiisha makundi makubwa ya watu kukusanyika kuzunguka mji mkongwe.
Watu walijenga mahema au kulala chini ya minazi huku wakisubiri ufunguaji wa
sherehe wakati wa asubuhi. Baadhi ya makundi ya watu yalikuwa ni makundi ya
vijana, baadhi ya vijana hawa walikuwa ni wafuasi wa mwanasiasa aliyejulikana
kwa jina la John Okello. Suali la
wafuasi wangapi walimfuata Okello katika mapinduzi hili ni suali la kutatanisha.
Kwa
hakika mwishoni mwa siku hiyo maelfu ya watu walijiunga na mapinduzi hayo baada
ya kujulikana matokeo. Ni kweli kwamba, inasemekana kwamba Jemedari Mkuu Okello
alikuwa na askari bataliani nne dhidi ya majeshi ya serikali usiku huo wa
mapinduzi, lakini Jee, walikuwa watu wangapi wanapohisabiwa?
Okello
aliarifu kwamba mapinduzi yalianza usiku wa manane pale alipoachana na askari
mia mbili na khamsini wa batalioni yake ya nne kwenye kambi ya Polisi ya Ziwani
na ghala ya silaha. Saa tisa usiku
alimrisha watu wake kukata waya wa ngome ya ziwani. Hilo lilikuwa tendo la mwanzo halisi la
Kimapinduzi na lilisaidia kuwajua washiriki halisi wa Kimapinduzi.
("Separate the men from the boys").
Okello aliarifu juu ya watu wake wakati huo". Ukubwa wa kikwazo chetu ulikuwa wazi
kwao. Tulikuwa tumejizatiti kwa mapanga,
mikuki na vyuma vya magari na ulikuwa tunabahatisha kupambana uso kwa uso na
askari waliosheheni bunduki za rashasha...." Wote waliondoka au kukataa
kutambaa kupitia kwenye waya isipokuwa watu arubaini tu.
Watu
arubaini hawa ndio walioikamata Zanzibar na kuuangusha utawala wa Kisultani na
zaidi ya miaka mia moja na thalathini na tatu kupitia masultani 12.
Wanamapinduzi
hawa walitambaa kiasi cha mita 25 ndani ya kambi ya Ziwani. Ndani walikuwepo maishirini ya maaskari. Askari hawa kama walivyo watu wengi wenye
busara Zanzibar walikuwa wamelala ghorofa ya juu ambayo pepo baridi za bahari
ziliweza kupoza/kuburudisha misitu ya joto.
Askari wawili tu walikuwa macho na walikuwa wanashika zamu ya ulinzi
chini.
John
Okello na askari wake waliwavamia walinzi hawa.
Bunduki za rashasha zililia na watatu kati ya askari batalioni ya nne
waliuliwa. Juu ya hivyo mmoja wa walinzi
pia aliuawa, alimalizwa na mshale uliolengwa na Mwana Mapinduzi aliyeitwa
Albert. Hapo tena Okello alikuwa uso kwa
uso na mlinzi aliyebakia, ilikuwa hapa ndipo utabiri wa ushindi wa Mapinduzi
ulipatikana. Watu hawa wawili
walitwangana, Jemedari Mkuu anatwambia hivi" Nilimpokonya
bunduki, tulipigana na kufanikiwa kumpiga tako la bunduki
shavuni" Upigaji risasi
ulisimama. Watu wa Jemedari Mkuu walikuwa tayari wamefika kwenye
malango ya chumba cha silaha ambamo
mamia ya Silaha za kisasa na maelfu ya risasi na baruti zilikuwa
zimefungiwa. Askari wasiokuwa na silaha
waliokuwa ghorofa ya juu, walijaribu kuteremka chini kwa fujo kwa kutumia ngazi
moja tu ya nje huku wakiwa wamejaa wasiwasi.
(kwa kudhibiti hali ya amani na utulivu ya kawaida, silaha zote
hufungiwa kwa ajili ya kuzihifadhi wakati maofisa wa Polisi wanapokuwa hawapo kazini). Askari wa batalioni ya nne ya Okello
walivurumisha mvua ya mikuki, mishale na mawe kwa askari walioduvaa na askari
hawa wa Serikali walilundikana wenyewe
katika ngazi nyembamba. Bunduki
aliyoihodhi Okello ambayo ilikuwa na risasi tatu ilitumika kulengea
risasi. Polisi hawa walirudi
ghorofa ya juu kutafuta kamba ya
kushukia kwa kupitia dirishani.
Ilikuwa tayari wamechelewa, milango
ya Chumba cha kuhifadhia silaha ilikuwa imevunjwa na Batalioni ya lnne
walivamia ndani. Mara tu kila mmoja
alikuwa yatari amesheheni bundundi ya rashasha.
Wapiganiaji uhuru hawa ambao
walianza usiku kwa silaha za vyuma vya magari zilizochongwa, sasa walikuwa ni
jeshi lilsheheni silaha nzuri na bora.
Askari hawa waliwasha moto wa ndege kwenye vyumba vya ghorofa ya juu na
mara tu polisi waliobakia walisalimu amri.
Askari wa Sultani walijaribu
kujilinda vikali dhidi ya waasi hawa.
Kikosi cha askari maalum chenye gari zenye kasi cha kukamata wahalifu
kiliwasili kiasi cha saa baada ya ngome ya ziwani kukamatwa na wanamapinduzi. Askari hawa 75 walikuwa na bunduki nyepesi na
walikuwa hawalingani na batalioni iliyosheheni silaha na iliyojidhatiti ndani
ya ngome ya silaha. Waasisi waliachia
askari wa Sultani kukaribia na baadae kuwa vurumishia mvua ya risasi. Mashambulizi yalikuwa makali sana hadi
vichaka vya karibu vilishika moto,
Polisi wa Sultani walirudi nyuma huku wakiwa wamekata tamaa.
Kwa kutumia kituo chao hiki kipya, wanamapinduzi
walitawanya bunduki kwa batalioni
nyengine tatu (ambazo tayari zilikuwa zimeshazizunguka sehemu muhimu lakini
bado kuzishambulia. Kwa amri ya mara
moja vituo vyengine vya Polisi na mawasiliano vilishambuli na kukamatwa. Upinzani mkubwa ulikuwa kituo cha Polisi cha
Malindi, ambapo hadi asubuhi lmilio ya risasi ilisikika.
Lakini juu ya hivyo hadi mchana
Sultani alikuwa ameshakimbia nchi,
iliyobakia ni historia tu.
Na Barghash 2001 Barghash@msn.com
0 comments: