MAKUBWA,. MTUHUMIWA ATUMA PICHA POLISI AKIDAI PICHA WANAYOTUMIA KUMTAFUTA HAINA MWONEKANO MZURI.
Mshukiwa anayesakwa atumia polisi 'selfie'
Mwanamume anayesakwa kwa makosa la kuteketeza na kuharibu mali ametuma picha ya selfie kwa maafisa wa polisi akisema picha iliyotumiwa na maafisa hao katika tangazo la kutafutwa kwake haikuwa ya kupendeza.
Donald "Chip" Pugh aliwatumia maafisa wa polisi picha aliyojipiga mwenyewe na kuandika ujumbe unaosema: "Hii hapa picha yangu nzuri, hiyo mliyotumia ni mbaya sana”.
Polise katika mji wa Lima, jimbo la Ohio, walikuwa wamepakia picha kwenye ukurasa wao wa Facebook wakiomba msaada wa kumtafuta Bw Pugh.
"Picha hii ilitumwa na Bw Pugh mwenyewe," kituo cha polisi cha Lima kiliandika kwenye ukurasa wa Facebook.
"Tunamshukuru kwa msaada wake lakini sasa tungeshukuru hata zaidi kama angejitokeza na kuzungumza nasi katika kituo cha polisi kuhusiana na mashtaka yanayomkabili. "
Polisi walisema anatafutwa kwa mashtaka kadhaa na amri ya kukamatwa kwake inahusiana na kushindwa kufika kituo cha polisi kama ilivyoagizwa.
"Bwana, walinikosea," Bw Pugh aliambia kituo cha Redio cha Ohio, akieleza ni kwa nini akawatumia polisi picha hiyo ya selfie.
"Waliweka picha iliyofanya nionekane vibaya kama vile Thundercat... au James Brown anayetoroka. Siwezi kufanya hivyo."
Ukarasa wa Facebook unaoitwa "Free Chip Pugh" umefunguliwa kufanyia suala hilo mzaha.
chanzo:bbcswahili
0 comments: