MWANAUME MFUPI KAMBI YA WAKIMBIZI ALIYETOROKA SOMALIA

...................

Mwanamume mfupi zaidi kambi ya wakimbizi


Somalia
Image captionAbdullahi alitoroka Somalia miaka kumi iliyopita
Katika kambi ya wakimbizi ya Hagardera kaskazini mashariki mwa Kenya, utampata mwanamume mfupi kwa kimo anayefuatwa sana na watoto.
Labda kwa kudhani kwamba ni mmoja wao, lakini ana tofauti kwani ana ndevu na umri wake pia ni mkubwa.
Sauti yake pia ni nzito.
Huyu ni Mirr Abdullahi, mwanamume mwenye umri wa miaka 40 aliyekimbia mapigano Somalia miaka kumi iliyopita.
Amekuwa akiishi pamoja na wakimbizi wengine katika kambi hiyo ambayo ni moja ya kambi tatu ambazo kwa pamoja hujulikana kama kambi za wakimbizi za Dadaab.
Amemwambia mwandishi wa BBC Bashkas Jugsodaay kwamba changamoto kuu anayokumbana nayo kambini ni kwamba watu humfanyia mzaha. Watoto pia humfuata kila aendako.
Kutokana na upweke, yeye hutumia muda wake mwingi akitafuna miraa na kuvuta sigara.
Pesa hupata kutoka kwa wahisani kambini.
Wakimbizi wengine wanapopanga kurejea Somalia, Abdullahi hana mpango kama huo.
Anasema akirudi huko, ana wasiwasi kwamba hali ikiwa mbaya hawezi kukimbia na kutoroka kama watu wengine

CHANZO:BBCSWAHILI
http://3.bp.blogspot.com/-e0QpO-QtZzE/U5DWDUZasXI/AAAAAAAABWg/QlFF97gwNdc/s1600/RAHA+GIF.gif
GIVE YOUR OPINIONS HERE

0 comments: