ONYO LATOLEWA KUHUSU KUSHIKA MIMBA
Bofya hapa KUTOKA BBCSWAHILI
Ushauri huu, kutoka kwa naibu waziri wa afya wa El Salvador Eduardo Espinoza, huenda ikawa hatua kali zaidi iliyochukuliwa na nchi za kanda hiyo kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo ambao unaaminika kusababisha watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo kuliko kawaida.
Virusi vya Zika, vinavyobebwa na mbu, vinadaiwa kuathiri vijusi vikiwa tumboni mwa kina mama walioambukizwa.
Virusi hivyo kwa sasa vimeathiri nchi nyingi Amerika. Umeelezwa kuwa mlipuko unaoendelea.
Kwa hivyo, kuwashauri wanawake kutoshika mimba ni jambo ambalo limeanza kuwa kawaida katika bara hilo.
Nchini Jamaica kwa mfano, wanawake wameshauriwa kuahirisha kushika mimba kwa angalau miezi sita.
Waziri wa afya Horace Dalley anasema ni muda tu kabla ya virusi hivyo kufika visiwani humo, kwa kuwa tayari kuna kisa cha maambukizi kimethibitishwa taifa jirani la Haiti.
.
Zaidi soma hapa
“Msishike mimba sasa”, mataifa yashauri wanawake
Mlipuko wa virusi
vinavyoaminika kusababisha watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo
kuliko kawaida vimezifanya serikali Amerika Kusini kuwashauri watu
kupanga uzazi.
"Tungependa kuwashauri wanawake wote wenye uwezo wa
kuzaa wachukue hatua kupanga uzazi, na wazuie kushika mimba kati ya
mwaka huu na mwaka ujao.”Ushauri huu, kutoka kwa naibu waziri wa afya wa El Salvador Eduardo Espinoza, huenda ikawa hatua kali zaidi iliyochukuliwa na nchi za kanda hiyo kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo ambao unaaminika kusababisha watoto kuzaliwa wakiwa na vichwa vidogo kuliko kawaida.

0 comments: